BLATTER AWAPONGEZA AZAM KUTWAA `NDOO` YA LIGI KUU!!

Sepp-Blatter-FIFa-580Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Sepp Blatter ametuma salamu za pongezi kwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC.

Blatter ameandika barua hiyo kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na kutoa pongezi hizo.
Amewapongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutokana na kuweka rekodi mpya ya bingwa tofauti.

Malinzi amethibitisha kupokea barua hiyo ya Blatter na kusema atawakabidhi Azam FC, kesho.

Aidha, Malinzi naye ametuma pongezi hizo za ubingwa kwa Azam FC.

“Tutawakabidhi barua hiyo ya Blatter kutoka Fifa, lakini tunawapongeza kutokana na kutwaa ubingwa,” alisema Malinzi.

Pongezi za Blatter kwa Azam FC ni za kwanza kwa rais huyo wa fifa kwa klabu iliyotwaa ubingwa Tanzania

UCHAMBUZI WA MECHI ZA KUFUNGA PAZIA LIGI KUU BARA HUU HAPA!!

IMG_8659Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar Es Salaam

0712461976

MICHUANO ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia tamati leo (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam fc wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.

Mechi zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni.

Mtandao huu unajaribu kukupatia tathmini ya mechi zote saba zikazopigwa leo hii.

YANGA SC VS SIMBA SC

Mechi hii haina mchecheto sana kwasababu timu zote zimeshapoteza nafasi ya ubingwa, japokuwa lengo kubwa leo hii ni kutafuta heshima kwa klabu zote.

Simba wamefanya vibaya msimu huu na kuelekea kuishia nafasi ya nne ambayo inategemeana na matokeo watakayopata dhidi ya Yanga, wakati huo huo matokeo ya Kagera Sugar waliopo nyuma yao yakisubiriwa huko Mkwakwani.

Simba wamecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 37 katika nafasi ya nne, wakati Yanga wapo nafasi ya pili kwa pointi 55 kwa kucheza mechi 25.

Endapo Yanga watashinda leo, basi watafikisha pointi 58, lakini hazitawasaidia kitu zaidi ya kulinda heshima,  kwasababu Azam fc walishazivuka na kuchukua taji msimu huu.

Kwa mazingira haya matokeo ya ushindi kwa timu yoyote hayatakuwa na maana hususani kwa Yanga, lakini angalau Simba yanaweza kuwahakikishia kushika nafasi ya nne.

Makocha wa timu hizi, Dravko  Logarusic ( Simba) na Hans Van der Pluijm ( Yanga) wanakutana kwa mara ya kwanza katika mechi ya watani wa jadi.

Lakini Loga aliwashawahi kuonja raha ya ushindi desemba 21 mwaka jana baada ya kuwafunga Yanga mabao 3-1 kwenye mechi ya `Nani Mtani Jembe`.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

WACHINA WAKAMATWA NA MAKOMBE FEKI YA KOMBE LA DUNIA ZAIDI YA 1,000

article-2606822-1D27D1F700000578-902_634x420
NDOTO ya mashabiki wa timu ya Taifa ya England `Simba watatu` ni kunyanyua kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
 Lakini suala hili limechukua sura mpya na shukurani za dhati ziwaendee viongozi wa desturi wa China waliofanikisha kukamata mzigo feki.
 Nchi ya China imekamata makombe feki ya kombe la dunia zaidi ya elfu moja ( 1,000) katika ghala ya kampuni moja kubwa ya usafirishaji nchini humo.
 Makombe hayo feki 1, 020  ya kombe la dunia yamekamatwa katika mji wa Yiwu, jimbo la Zhejiang, ambalo ni moja ya miji mikubwa ya usafirishaji wa bidhaa duniani.
 Makombe hayo feki kwa asilimia kubwa yanafanana na makombe halisi ya FIFA na yalikuwa tayari kusafirishwa kwenda nchini Libya.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MJINI UNGUJA KUFUNGUA KONGAMANO LA MUUNGANO KESHO.

1(14) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Wa pili (kulia) ni mkewe Mama Zakia Bilal. Picha na OMR

2(12)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya maafisa na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mjini Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kufungua rasmi Kongamano la Muungano, linaloanza kesho katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort. Picha na OMR

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA YA IJUMAA KUU

2 (9) Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu3 (14)Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam jana. 

4 (8) Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa akiwa katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT  la Azania Front Dar es Salaam.

6 (5)Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Porkap Kadinali Pengo akiubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Josef Dar es Salaam jana.

7 (3) Waumuni wa Kanisa la Mtakatif Josef Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika Dar es Salaam jana.

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAENDELEZA UBABE MICHUANO YA MEI MOSI MOROGORO

_DSC0941Jonathan  Tossi  Jeshi la  polisi  

Mabigwa  wa  tetezi  wa  michuano  ya  mei mosi  timu  ya  wizara  ya  mambo  ya  ndani  imeendelea  kutetea  ubigwa  wake   kwa  Kuicharaza  timu  ya   kampuni  ya  tumbaku  mkoani  morogoro  (TTPL)  goli  nne kwa bila  mabao  ambayo  yalipatika  katika  vipindi  vyote  viwili  vya  mchezo  huo .

Mabao  yote  hayo   yalipachikwa  wavuni  na  wachezaji   Adrew  Paul   bao  la kwanza  dakika  ya  kumi tano  ya mchezo  na bao lapili  likipachikwa  wavuni  na Pascal  Maige  dakika  ya ishirini  na  tano  ya  mchezo pia ,bao latatu likitiwa  nyavuni  na Weston  Wanjara    mnamo  dakika  ya therasini  na  tano  ya  mchezo  kipindi  cha  kwanza na  bao  la  mwisho  likifungwa  na John  Kanakamfumu   dakika  ya  therasini  na  tisa  ya  mchezo  kipindi  cha  pili.

Aisha  katika  mchezo  wa  mpila  wa  pete  timu  ya  wanawake   wizara  ya  mambo  ya  ndani  nchi  nayo  imeendeleza  ubabe   kwa  kuibungiza  timu  hiyohiyo   ya  kampuni ya  tumbaku  mkoani  morogoro  jumla  ya    magori  34  kwa  15   katika  michuano   hiyo  ya  mai  mosi  ilianza    mkoani  morogoro  katika  uwanja  wa Jamhuri   huku  mfungaji  wa  magori  kati seti za  mchezi  akiwa  Bi Ndegawako wa  wizara  ya  mambo ya  ndani,wakati  kwa  kampuni  ya  tumbaku  morogoro  mfungamagori  hayo  kwa  seti  zote  Bi   Asha  Juma .

 Pamoja   na  hayo pia  timu  ya kuvuta kamba  ya wanaume toka  wizara  ya  mambo ya ndani   imepoteza  mchezo  wake  kwa  kuvutwa   na   Wizara  ya  uchukuzi  kwa  seti zote mbili  huku  timu ya wanawake   mambo ya ndani  ikiibuka  na  ushindi  kwa  mivuto  yote  miwili  aidha  mashindano  hayo  yanaendelea  hapa  Mkoani  Morogoro 

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA ELIMU

IMG_9946Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar jana jioni, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

IMG_9940Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MABINGWA AZAM FC WAWAFARIJI WATOTO YATIMA CHAMAZI!!

boko na sure (1)Nahodha wa Azam FC, John Bocco kulia akiwa na Msaidizi wake, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wakikabidhi seti ya king’amuzi cha Azam TV kwa viongozi wa Yatima Group kushoto leo mchana

………………………………………………….
 
WACHEZAJI wa klabu ya Azam FC mchana wa leo wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima, kijulikanacho kama Yatima Group Trust Fund, kilichopo Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabingwa hao wapya wa Bara walifika katika kituo hicho baada ya sala ya Ijumaa wakiongozwa na Mkuu wa msafara, Katibu wa timu, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ na kukabidhi misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na jezi, seti ya king’amuzi cha Azam TV na dishi lake, na vyakula na vinywaji.
Pamoja na hayo, wachezaji wa Azam FC walionyesha upendo kwa watoto hao kwa kujumuika nao na kufurahi pamoja. Watoto hao walijibu kwa kushangilia ‘Azam Azam’.
Mmoja wa Maofisa wa kituo hicho, akitoa hutuba yake kwa msafara wa Azam, inayomilikiwa na kampuni ya Bakhresa Group Limited, alishukuru kwa ujio huo na akasema kituo hicho ni mashabiki wakubwa wa Azam na siku zote wamekuwa wakiunga mkono timu hiyo na sasa wanafurahia mafanikio yake.
Alisema kampuni ya Bakhresa Group inayomilikiwa na Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake ni miongoni mwa wafadhili wakubwa wa kituo hicho.
kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

PIGO CHELSEA: HAZARD KUWAKOSA ATLETICO UEFA!!

388495_heroaWINGA machachari wa Chelsea, Eden Hazard yuko hatarini kukosa mechi ya kwanza ya nusu fainali ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Hazard alitolewa katika mchezo wa robo fainali dhidi ya PSG ambapo walishinda mabao 2-0 na kufuzu nusu fainali kwa wastani wa mabao 3-3, lakini Chelsea walikuwa na faida ya bao la ugenini.

Kocha msaidizi wa Chelsea Steve Holland mapema wiki hii alisema Hazard anaendelea vizuri na anaweza kucheza, lakini taarifa za leo ijumaa ni mbaya zaidi kwasababu nyota huyo hatakuwa fiti kwa mechi hiyo.

“Sio kwamba Hazard hataweza kuimarika, lakini kushindwa kufanya mazoezi na timu inaashiria wasiwasi kwa yeye kucheza”. Alisema taarifa ya Holland kwa waandishi wa habari.

Kabla ya kwenda kucheza nusu fainali ya UEFA katika uwanja wa Vicente Calderon, Chelsea watasafiri kuwafuata vibonde wa ligi kuu soka nchini England, klabu ya Sunderland, mechi inayoaminika kuweka wazi kama Mourinho ataendelea kuwepo katika mbio za ubingwa.

Katikati ya wiki, mashabiki wa soka walishuhudia Sunderland wakiwakazia Manchester City na kutoka sare ya 2-2, lakini kama Chelsea watashinda mechi hiyo na nyingine zote zilizobaki wanaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kubeba mwari.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

GUARDIOLA AKIRI BAYERN KUSHUKA KIWANGO, AONGEZA DOZI YA KUWAKABILI REAL MADRID UEFA!!

392295_heroaBAADA ya kulaumiwa kuwa kiwango cha Bayern Munich kimeshuka kwa siku za karibuni, kocha mkuu Pep Gaurdiola anaamini timu yake itarudi katika kiwango chake dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Guardiola amewasifu vijana wake kwa kuonesha kiwango kizuri katika mazoezi, na kusema kuwa watarudisha makali yao ya msimu uliopita katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu.

Kikosi cha Bayern tayari kimeshafanikiwa kutwaa ubingwa wa Bundesliga na sasa kinaliwinda kombe la UEFA na DFB-Pokal.

Wakitokea katika mafanikio ya kuwatoa Manchester United robo fainali ya UEFA, Bayern walikula kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa ligi dhidi ya  Borussia Dortmund jumamosi iliyopita .

Pia wakitokea katika mafanikio ya kufuzu fainali ya DFB-Pokal kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Kaiserslautern katikati ya wiki, Bayern watawavaa Eintracht Braunschweig katika mchezo wa ligi kabla ya kukabiliana na Real Madrid wiki ijayo.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Ali Hassani Mwinyi atembelea banda la Mamlaka ya usafiri wa anga

01Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi  akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo  katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

02Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi  akimsikiliza kwa makini Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo  katika Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 03Rais Msaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi akikabidhiwa nyaraka na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chach,zenye ujumbe wa shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati alipotembelea katika banda la Mamlaka hiyo kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka katika  Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

MAMA SALMA APOKEA MBIO ZA PIKIPIKI KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUNGANO-ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI

IMG_7991 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wa Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini mtoto Idd Omar kutoka katika Kijiji cha Madangwa , kata ya Sudi huko Lindi Vijijini. Mama Salma alifika kijijini hapo kwa ajili ya kupokea mbio za uzalendo za pikipiki zilizoandaliwa na Umoja wa Vijana, (UVCCM) kitaifa zikitokea Mkoa wa Mtwara tarehe 17.4.2014.

IMG_8008Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaelekeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Madangwa namna ya kushika mfagio ili usiweze kuleta madhara kwa watoto waliobeba na hata wengine na pia ni njia bora ya kulinda afya zao kwani wakishika upande unaotumika kufagia wanaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa.  IMG_8023Baadhi ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014. IMG_8035Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Said Sinani (mwenye kofia) akifuatana na viongozi wenzake wa Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Vijana kwenda kukabidhi mbio za pikipiki kwa uongozi wa Mkoa wa Lindi kwenye Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014.

IMG_8090 Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara ndugu Mohamed Sinani  akikabidhi picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa na picha ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mheshimiwa Abeid Aman Karume kwa Mama Salma Kikwete kuashiria muendelezo wa mbio za uzalendo za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar hapo tarehe 26.4.2014. IMG_8091Mjumbe wa NEC wa Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Madangwa na wageni waliohudhuria sherehe ya kupokea mbio za pikipiki kwa Mikoa ya Kanda ya Kusini inayojumuisha Ruvuma, Mtwara na Lindi katika kusherehekea miaka 50 ya Mungano. IMG_8109H IMG_8121Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mingoyo wakati wa sherehe ya mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano zitakazofikia kilele tarehe 26.4.2014. IMG_8146Viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiana mbio za pikipiki kusherehekea miaka 50 ya Mungano. IMG_8209Bwana Salum Musa Mtungulu mkazi wa Kijiji cha Madangwa alitumia fursa hiyo ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kurejea Chama Cha Mapinduzi akitokea Chama Cha NCCR- Mageuzi. Katika picha hiyo anatoa maelezo  ya kitendo hicho huku makada wakimvisha mavazi ya Chama Cha Mapinduzi. IMG_8247Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM kutoka Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mnazi Mmoja  kilichoko katika Kata ya Mingoyo walifurika kushuhudia sherehe za mbio za pikipiki za uzalendo kusherehekea miaka 50 ya Mungano . IMG_8266 Baadhi ya wasichana na akina mama wakionyesha umahiri wao katika kucheza ngoma za utamaduni wakati wa sherehe ya makabidhiano ya mbio za pikipiki kutoka mkoani Mtwara kwenda Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Madangwa tarehe 17.4.2014. IMG_8448Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Seleman Salum Namputa, miezi 3, aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine. Kulia ni Mama mzazi wa mtoto Seleman ajulikanaye kama Mariam kutoka katika kijiji cha Moka huko Lindi Vijijini. Mama Salma alitembelea hopitalini hapo tarehe 18.4.2014.

 PICHA NA JOHN LUKUWI.  

Muungano bado uko imara – Mzee Mwinyi

1Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa Bunge Bwana Patson Sobha, wakati alipowasili kwenye Banda la Bunge la maonesho ya maadhisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania yanayoendelea katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Maonesho hayo yatakayofikia kilele siku ya Jumamosi Aprili 19, ikiwa ni maandalizi ya siku kuu ya Muungano ambayo huherekewa Aprili 26 kila mwaka. 2Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi akikabidhiwa  zawadi ya vitabu na nyaraka mbalimbali za Bunge na Bi. Devotha George alipotembelea banda la Ofisi ya Bunge kwenye Maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

tff_LOGO1

PAZIA VPL LAFUNGWA, AZAM KUKABIDHIWA KOMBE CHAMAZI

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.

Mechi zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake ni sh. 7,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.

Tayari tiketi zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu), Buguruni Shell, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo OilCom, Dar Live Mbagala na Uwanja wa Taifa.

Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Oljoro JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Coastal Union na Kagera Sugar (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga).

MICHUANO YA BEACH SOCCER KUANZA JUMAPILI

Michuano ya mpira wa miguu ya ufukweni (Beach Soccer) inazinduliwa rasmi keshokutwa (Aprili 20 mwaka huu) kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam na kushirikisha timu 13.

Uzinduzi huo utaanza saa 5 asubuhi na mechi zitachezwa hadi saa 11 jioni. Michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini inashirikisha timu 13 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Ardhi (AU), Chuo Kikuu cha St. Joseph Tanzania (SJUIT), Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO), Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Vingine ni Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Utawala wa Kodi (ITA) na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Michuano hiyo itakuwa inachezwa Jumamosi na Jumapili kwenye fukwe za Escape One na Gorilla Beach iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam.

WAZOEFU TAIFA STARS KUTAJWA KESHO

Wachezaji wazoefu wa Taifa Stars watakaoungana na wale 16 waliopatikana katika mpango wa maboresho wa timu hiyo watatangazwa kesho (Aprili 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itapiga kambi kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wachezaji waliopatikana katika mpango wa maboresho ya Stars wanatarajiwa kuwasili leo (Aprili 18 mwaka huu), na kwenda moja kwa moja kambini kuwasubiri wenzao watakaotajwa kesho (Aprili 19 mwaka huu).

Wachezaji hao ni kipa Benedicto Tinoko Simwanda (Mara), Emma Namwondo Simwanda (Temeke), Joram Nason Mgeveje (Iringa), Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala), Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke) na Said Juma Ally (Mjini Magharibi).

Wengine ni Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara), Chunga Said Zito (Manyara), Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi) na Paul Michael Bundara (Ilala).

TANZANIA NI NCHI YA AMANI

Vijana watakiwa kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili waweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha

IMG_3981Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
 Vijana mkoani Lindi wametakiwa kuacha tabia ya kuilalamika Serikali kuwa maisha ni magumu bali watumie  fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Mwito huo umetolewa jana na Mjumbe wa Baraza kuu na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCC) taifa kutoka mkoa wa Lindi Jabiri Makame kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha   Mnazi mmoja wilaya ya Lindi Mjini kwa ajili ya kuzipokea mbio za kizalendo za pikipiki na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Jabiri alisema  vijana wengi wamekuwa wakiilalamika Serikali kutokana na changamoto zinazowakabili na kusahau kuwa kazi ya Serikali ni hakikisha kwamba inawaandalia mazingira mazuri ya wao kuweza kujikwamua kiuchumi  na kuweza kujiletea maendeleo hii ni pamoja na kuwapatia mikopo .

“Halmashauri zetu zinatakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kinamama na vijana naamini hata Halmashauri za mkoa huu zinafanya hivyo lakini fedha hizo hazitolewi kiholela ni lazima wahusika wajiunge  katika makundi yaliyosajiliwa  kwa mfano  kundi la madereva wa bodaboda, bajaji, kina mama lishe na vikundi vya mpira pia vinaweza kuwa vya ujasiriamali na kuweza kupata mkopo ambao watautumia katika shughuli zao za maendeleo”, alisema Jabiri.

Kuhusu suala la uongozi alisema Rais Kikwete anawaamini sana vijana na ndiyo maana amewateua na kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na Serikali na kutoa mfano wa mawaziri na wakuu wa wilaya. 

Jabiri alisisistiza, “Katika uchaguzi unaokuja wa Serikali za Mitaa  na Uchaguzi mkuu mwakani vijana wa CCM msiogope kuomba nafasi za uongozi  wakati ukifika wajitokeze kuchukuwa fursa za uongozi jambo la muhimu ni kutotangaza  nia mapema subirini hadi wakati utakapofika”.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo aliwapongeza UVCCM kwa kuandaa mbio hizo za uzalendo kwani ni ukweli usiopingika kuwa Muungano wenye dhana ya kizalendo na historia ya nchi unatimiza miaka 50 tarehe 26/4/2014.

Mama Kikwete alisema, “Leo hii nchi kubwa zenye nguvu kiuchumi Duniani zinazungumzia suala la kuungana ili kuimarisha nguvu yao ya pamoja , kwanini sisi tukubali kutengana? Muungano wetu ni kigezo kizuri ndani ya Bara la Afrika  na kote Duniani tusikubali kamwe kuuvunja jambo kubwa hapa na la msingi ni kukaa kwa pamoja na kujadili hatimaye kupata ufumbuzi yakinifu”.

MNEC huyo alisema vijana wa CCM ndiyo wanaotegemewa kuwa viongozi hapo baadaye, walipoona kuna watu wanataka kupotosha ukweli juu ya umuhimu na faida za kuwa na muundo wa Serikali mbili wakaamua kuzunguka nchi nzima na kuunga mkono umuhimu wa nchi kuwa na Serikali mbili na siyo moja wala tatu kama vinavyotaka vyama vingine vya Siasa.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally  Mtopa alisema Mwenyezi Mungu amemuumba binadamu katika umbo la mapenzi na  kumpa akili ya kuweza kuchagua lipi alifuate kati ya jema na baya hivyo ni muhimu kwao kuweza kuamua ni chama gani cha kuweza kuingia na siyo kukurupuka.

“Sisi wanachama wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Lindi na Tanzania nzima tunaunga mkono muundo wa Serikali mbili na kuwepo kwa muungano ambao umetuletea manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na watu kutoka Tanzania bara na Visiwani kuishi pamoja kwa amani na upendo”, alisema Mzee Mtopa.

UVCC mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara waliandaa mbio za uzalendo za pikipiki zenye kauli mbiu Miaka 50 ya Muungano Dumisha Muungano, vijana tutumie fursa zilizopo katika maeneo yetu. Tanzania kwanza mengine baadaye ambazo zilizinduliwa mkoani Ruvuma katika wilaya ya Namtumbo tarehe 13/4/2014 kumalizika mkoani Lindi tarehe 17/4/2014.

Mkoa wa Lindi ulizipokea mbio hizo kutoka kwa UVCCM mkoa wa Mtwara makabidhiano yaliyofanyika kata ya Madangwa na katika mkutano wa hadhara uliofanyika hapo jumla ya wanachama watatu walijiunga na Chama hicho wawili kutoka chama cha Civic United Front (CUF) na mmoja kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .

Lengo la mbio hizo ni kuwaenzi waaasisi wa Taifa la Tanzania  ambao ni Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuwafikishia ujumbe watanzania  juu ya umuhimu wa muungano na kuwaeleza wapi ulipotoka, ulipo na unakokwenda na vijana kutumia fursa zilizopo kujiedeleza.

Katika mkutano huo jumla ya wanachama wapya vijana 19 walijiunga na umoja huo, mmoja alirudisha  kadi ya uanachama wa CHADEMA na kujiunga na chama hicho.

LIGI KUU: SIMBA VS YANGA, AZAM VS JKT RUVU, PRISONS VS ASHANTI MECHI TAMU, RATIBA NZIMA HII HAPA!!

IMG_3703Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar Es Salaam

0712461976

PAZIA la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 linafungwa kesho aprili 19 kwa timu zote 14 kushuka uwanjani katika miji tofauti nchini.

Ligi inamalizika kesho wakati timu tatu zimeshajihakikishia nafasi tatu za juu.

Azam fc wametwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na klabu yoyote.

Yanga wamechukua nafasi ya pili wakiwa na pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote chini yake.

Mbeya City nao wameshika nafasi ya tatu kwa pointi 46 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya chini yake.

Simba sc wao wao wapo mbioni kuisaka nafasi ya nne kwa pointi zao 37 baada ya kucheza mechi 25.

Nafasi ya tano wapo Kagera Sugar wenye pointi 35, na endapo Simba watafungwa kesho na wao wakashinda, basi Mnyama anaweza kumaliza ligi katika nafasi ya tano.

Katika mechi zote 7 hapo kesho, mechi tatu pekee  zina  hamasa kubwa kwa mashabiki wa soka nchini.

Mechi ya kwanza iliyovuta hisia za mashabiki wa soka ni ile ya Yanga dhidi ya Simba sc ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Timu hizi zitakutana zikiwa na mafanikio tofauti msimu huu ambapo Yanga wameambulia nafasi ya pili, huku Mnyama akijikongoja katika nafasi ya nne.

Simba na Yanga zinakutana jumamosi, huku Yanga wakiwazidi wenzao kwa mafanikio msimu huu.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

JUMUIYA YA MUZDALIFAT YASHIRIKIANA NA TAASISI YA I.H.H KUWAPA SADAKA WATOTO YATIMA

DSC_0579 Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat(Muzdalifat Islamic Charitable)wakishirikiana na Taasisi ya I.H.H kutoka uturuki,wakichuna mbuzi waliokwisha kuchinjwa kwa ajili ya sadaka kwa Watoto yatima hafla iliofanyika huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar. DSC_0595 Wawakilishi kutoka Taasisi ya I.H.H ya Uturuki wakisalimiana na wanafunzi chekechea wa Skuli ya Muzdalifat mara baada ya kushuka kwenye gari huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.DSC_0659Wawakilishi wa Taasisi ya I.H.H kutoka Uturuki wakigawa sadaka ya Unga,Mchele,Mafuta ya kupikia pamoja na Nyama kwa Watoto Yatima katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

DSC_0672Wawakilishi wa Taasisi ya I.H.H,kutoka Uturuki wakiendelea kugawa sadaka ya Vitu mbalimbali ikiwa pamoja na Unga wa Ngano,Mchele,Mafuta ya kupikia na Nyama kwa Watoto mayatima walio katika maeneo mbalimbali Zanzibar. 

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

KIAMA CHA KIBADENI, MWAMWAJA KESHO DIMBA LA JAMHURI MORO!!

IMG_1721Na Baraka Mpenja, Dar Es Salaam

ABDALLAH  Kibadeni  au David Mwamwaja, lazima mmoja aishushe daraja timu yake katika dimba la Jamhuri Mkoani Morogoro.
Maaafande wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons `Wajelajela` kesho wanahitimisha ligi kuu soka Tanzania bara kwa kukabiliana na wauza mitumba wa Ilala, Ashanti United uwanja wa Jamhuri.
Hii ni mechi ngumu mno na inahitaji maarifa makubwa kwa kocha wa Ashanti, Mzee Kibadeni na Mwamwaja wa Tanzania Prisons.
Kati ya timu hizi mbili, moja lazima iungane kushuka daraja na timu za JKT Oljoro ya Arusha na Rhino Rangers ya Tabora.
Timu zote zimecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 25. Kinachozitofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Prisons wamecheza mechi 25 ambapo wameshinda mechi 5, sare 10 na kupoteza mechi 10.
Wajelajela hao wamefumania nyavu mara 25 na kufungwa mabao 33. Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata hasi (-8).
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MACHAMPION AZAM FC KUANDIKA HISTORIA SAFI KESHO CHAMAZI!!

azam bingwaNa Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar Es Salaam

MABINGWA Azam fc wanatarajia kuandika historia hapo kesho kwa kutwaaa taji bila kupoteza mechi yoyote ambapo watakabiliana na JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex, Uliopo Chamazi, nje kidogo ya jijini la Dar es salaam.
Hii itakuwa mechi ya mwisho kwa Azam fc waliocheza mechi 25 mpaka sasa bila kufungwa.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog alisema kutwaa ubingwa ni mafanikio makubwa, lakini kuchukua mwari bila kufungwa mechi yoyote ni historia nzuri kwa klabu.
“Wachezaji wangu wasibweteke na ubingwa. Bado tuna mechi moja kesho dhidi ya JKT Ruvu. Nahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka rekodi nzuri”.
“Tutaingia kwa nguvu zote na kuhakikisha tunawafunga wapinzani wetu”. Alisema Omog.
Naye kocha mkuu wa JKT Ruvu Fredy Minziro alisema kikosi chake kimejiandaa kukabiliana na Azam fc kwa nguvu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

MZIMU WA AZAM WAMTESA MWAMBUSI, KESHO MBEYA CITY VS MGAMBO SOKOINE!!

DSC000681Na Baraka Mpenja wa fullshangwe, Dar es salaam

WASHINDI wa tatu msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya kesho jumamosi inatarajia kufunga pazia la ligi hiyo dhidi ya Maafande wa Mgambo JKT.

Hii itakuwa mechi muhimu kwa kocha mkuu wa klabu hiyo Juma Mwambusi kutokana na matokeo aliyoyapata wiki iliyopita dhidi ya Azam fc ambapo alifungwa mabao 2-1 nyumbani na kuwapa ubingwa rasmi.
Endapo Mwambusi atashinda mechi ya kesho, basi  itakuwa faraja kubwa kwake na kwa mashabiki wa klabu hiyo iliyoleta ushindani mkubwa mno msimu huu.
Mbeya City FC mpaka sasa wamecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 46 katika nafasi ya tatu ambayo tayari wamefanikiwa kuichukua.
Kwa upande wa Mgambo JKT, wanauchukulia mchezi huo kwa uzito wa hali ya juu ili kuweza kupata pointi tatu muhimu na kufikisha pointi 29.
Japokuwa maafande hawa wapo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 26 na kujiweka mazingira mazuri ya kubaki ligi kuu, lakini bado wanahitaji ushindi katika mechi ya kesho.
Kuelekea katika mchezo huo, kocha mkuu wa msaidizi wa Mgambo JKT, Moka Shaban Dihimba alisema kuwa wataingia kwa nia ya kupambana na kuibuka na ushindi dhidi ya Mbeya City wenye machungu ya kufungwa.
“Tunajua wapinzani wetu ni wazuri sana hasa wanapokuwa nyumbani kwao”.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blgospot.com

CHICHARITO AMWAMBIA MOYES ANATAKA KUONDOKA OLD TRAFFORD!!

377343_heroaUVUMILIVU umemshinda mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Javier Harnandez `Chicharito` na sasa ameitaka klabu yake kumuuza majira ya kiangazi mwaka huu baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Chicharito ameongea mara tatu na bosi wake David Moyes katika miezi miwili iliyopita juu ya yeye kunyimwa nafasi ya kucheza, huku akianzishwa katika mechi tano tu za ligi kuu msimu huu.

Nyota huyo raia wa Mexico ameiambia klabu yake kuwa atasikiliza ofa zikazokuja juu yake majira ya joto na hadhani kama yupo katika mipango ya Moyes hapo baadaye.

Chicharito ameshindwa kupata namba ya kudumu mbele ya Wayne Mark Rooney, Robin Van Persie na Danny Welbeck.

Sasa mshambuliaji huyo amefikia maamuzi ya kuondoka huku akihusishwa na mpango wa kuhamia Atletico Madrid kama mrithi wa Diego Costa mwenye kila dalili ya kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

BARCA NI SHIDA! NEYMAR, ALBA NJE WIKI NNE!!

388904_heroaMAJANGA BARCA!. Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa wiki nne, wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote kupata majeruhi.

Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata majeruhi ya mguu jana katika mchezo wa fainali ya kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.

Kinda huyo mwenye miaka 21 alishindwa kuisaidia Barca kuepukana na kipigo cha mabao 2-1, huku Mbrazil huyo akikosa nafasi ya wazi dakika za lala salama.

Neymar atakosa mechi zijazo dhidi ya Athletic Bilbao, Villarreal, Getafe na Elche.

Hata hivyo klabu ya Barca ina matumaini kuwa nyota wake huyo anaweza kurudi katika mechi ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid.

Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

POLISI YAWASHAURI WAFANYABIASHARA ARUSHA

MNGULUDCIJeshi la polisi limewataka wafanyabaishara wakubwa hasa wamiliki wa kumbi za starehe,Jiji la Arusha na Halmashauri zake zote kuhakikisha kuwa wanaweka vifaa vya kujihami (CCTV CAMERA) ili kuweza kugundua wanaotaka kusababisha milipuko ya mabomu.
Aidha kauli hiyo inakuja siku moja mara baada ya watu wasiofahamika kutega bomu katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Arusha Night Park, huku bomu lingine tena likiwa limetegwa katika baa nyingine ijulikanayo kama Washington Baa mapema juzi

Hayo yameelezwa mjini hapa na Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai Isaya  Mngulu wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Hali ya Arusha kukumbwa na milipuko ya mabomu ya mara kwa mara.

Alidai kuwa mpaka sasa takwimu zinajionesha kuwa tukio hilo linajirudiarudia sana na hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kuanzia sasa kwani hatamabomu ya kienyeji nayo yanatumika sana kuuua lakini pia kujerui watu

Alisema kuwa hata uongozi mzima wa mkoa wa Arusha nao unatakiwa kuhakikisha kuwa kuanzia sasa unaanza mikakati ya kufunga vifaa mbalimbali ambavyo vitakavyoweza kuwabaini wahalifu wote wa mabomu kwani uwezekano wa kuwatambua hata kupitia vifaa hivyo upo.

aliongeza kuwa wamiliki wa kumbi za starehee nao pia wachukue tahadhari kuanzia sasa ambapo wanatakiwa kulinda uhai wa wateja wao na kamwe wasijisahau ingawaje nao wanahitajika kuwa na vifaa vya kisasa hasa CCTV CAMERA ili kuharakisha zaidi upelelezi.
“kutokana na hali ya mabomu ilivyo kwa sasa ni muhimu sana kwa kila mtu kuweza kuchukua tahadhari ingawaje na sisi tutahakikisha  kuwa tunawalinda ipasavyo wananchi wetu na hatutaweza kuruhusu  tena Arusha ikapata na janga lingine la mabomu ingawaje pia tunaimarisha ulinzi kila kona hususani kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu”aliongeza Isaya 

Katika hatua nyingine alisema kuwa Jeshi la polisi Nchini limetangaza kitita cha Milioni 10 kwa mtu yeyote atakayewezesha kutoa taarifa sahihi na kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyesababisha mlipuko wa bomu katika nyumba ya kulala wageni (Arusha Night Park)
Alimalizia kwa kusema kuwa katika tukio hilo la kurushwa kwa bomu la kienyeji katika nyumba hiyo ya kulala wageni hali za majerui zinaendelea vizuri na kwa sasa majerui nane wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha.

MIHEWA AMSHANGAA DK SLAA

Dr-Wilbroad-Slaa-300x214

Na Gladness Mushi, Arusha
MJUMBE wa kamati kuu ya CCM, taifa, Abdalah Mihewa, amemshangaa ,Katibu mkuu wa Chadema, Dakta Wilbroad Slaa, kwa kubeza maendeleo yaliyopatikana jimboni Karatu.
 
Mihewa amesema hayo jana kwenye ofisi ya CCM, wilaya ya Karatu, baada ya kupokea salaam za Chama kutoka kwa katibu wa Chama wilatya ya Karastum, Elly Minja, na kusema kuwa,kiongozi huyo hana shukurani.
 
Mihewa ambae pia ni katibu wa CCM, mkoa wa Dar es  Salaam, aliyekuwa ziarani wilayani Ngorongoro, kusimamia uchaguzi wa viongozi wa baraza la Umoja wa vijana mkoa wa Arusha, amesema serikali ya CCM, imefanya mengi jimboni Karatu ikiwemo kujenga bara bara ya Lami kutoka Arusha hadi Lango kuu la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, pia serikali imetekeleza mradi mkubwa wa maji kwa wananchi wa Karatu jambo ambalo ni ukombozi mkubwa lakini Salaa bado anabeza kuwa hakuna kilichofanyika .
 
Amesema kuwa Serikali ya CCM, inahudumia watanzania wote bila kujali itikadi hata kama majimbo yanaongozwa na wapinzanilazima wananchi waliopo watapata huduma bila ya ubaguzi wala upendekleo.
 
Serikali ya CCM,inaboresha miundo mbinu nchini kote bila kujalilakini leo mtu mzima anaponda na kubeza huyo ana matatizo ya akili hata angelikuwa ni kipofu basi angelipapasa aone nini kilichofanywa na serikali ya CCM,jimboni humona sio kubeza
 
Akawataka viongozi na wananchi kuimarisha mshikamanona kujipanga kulikomboa jimbo hilo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi .
 
Awali  Katibu wa  CCM, Wilaya ya  Karatu, Elly Minja, katika salam zake amesema wananchi wilayani Karatu wamechoshwa na miaka 17 ya Chadema tangia kuchukua jimbbo hilo wamekwama kimaendeleo.
 
Amesem,a wananchi jimboni humo wanadai wameschoshwa na maneno bila vitendo sasa wanajiandaa kuking’oa chama cha Chadema, ili waweze kupata maendeleo kutoka Chama cha mapinduzi ambacho serikali yake inawapatia huduma mbalimbali ikiwemo mnradi mkubwa wa maji ambao limekuwa ni tatizo kubwa na la kudumu.
 
Amesem,a wananchi pia wamechoshwa kufanywa ngome ya Chadema,na sasa wameahidi katika uchaguzi mkuu ujao kukiondoa chama hicho cha Chadema..

UVCCM YAHAMASISHA SERIKALI MBILI MIKOANI

SAM_3508Baadhi ya viongozi wa ccm wakiwa katika picha ya pamoja sambambana picha za waasisi wa muungano katika ngome ya mkwawa iliyoko kalenga

Na Denis Mlowe,Iringa

 
KATIKA kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kimedhamiria kupitisha serikali mbili katika bunge maalum la katiba, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kukubaliana serikali mbili ambazo wamekuwa wakitumia mbio za pikipiki kueneza ujumbe huo kwa kutumia  jumuiya ya vijana wa chama hicho.
 
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Stand ya Mlandege juzi,Kiongozi wa mbio za pikipiki kitaifa, Hassan Bamboko alisema lengo za mbio hizo ni kufikisha ujumbe wa chama hicho kwa wananchi kuwa serikali mbili ndizo zitakazopitishwa na chama hicho na kuwataka wananchi kuuwanga mkono katika harakati hizo.
 
Alisema licha ya kuhamasisha ujumbe wa serikali mbili ambao wananchi wengi wamekuwa wakiukataa mbio hizo zinatumika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ambao nao uko mashakani kutokana na chama cha mapinduzi kuendelea kung’ang’ania serikali 2 badala ya tatu ambazo ni chaguo la wengi.
 
“Mbio hizi za pikipiki tunaenda nazo nchi nzima lengo nikuwaeleza wananchi kuwa serikali mbili zinatosha wanaotaka tatu wanauchu wa madaraka na ni mzigo kwa kweli na nawaomba muelewe hili kutokana na ni ya chama cha mapinduzi kwa wananchi wake kuwa ni nzuri katika kulinda usalama wa nchi” alisema Bamboko na kuongeza kuwa tuna miaka 50 tukiwa na Muungano wa serikali mbili licha ya kuwa na kasoro zilikuwa chache na kuongezeka zinaweza kurekebishwa na hakika serikali mbili zinatosha” alisisitiza.
 
Kwa upande wake kiongozi mwingine wa mbio za pikipiki,Seki Kasuga alisisitiza kuwa serikali mbili ndio mustakabali wa Watanzania katika maisha ya mbele  na wanaotaka kuugawa Muungano watafute kwanza udongo uliochanganywa ili ugawanywe.
 
Naye Katibu wa ccm wilaya ya Mufindi Miraji Mtaturu akizungumzia kuhusu muundo wa Serikali
Tatu alisema Chadema wanatumiwa na magaidi wa nchi za nje kutaka serikali tatu ili kuwavuruga
wananchi.
 
Aliwataka wananchi kumfikishia ujumbe Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe kuwa serikali tatu haikubaliki kwa Watanzania hivyo wanajidanganya kwa kuwa mwarubaini wa maendeleo ya Watanzania ni serikali mbili na sio tatu kama zinazoshinikizwa na wapinzani.
 
Na Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa Halawi Haidari mwenyeji wa Zanzibar, alisema
Wazanzibar wanautambua Muungano wa Serikali mbili hivyo hawawezi kutoka katika Muungano kwa sababu Wazanzibar wapo huru kuishi popote  katika ardhi ya Tanzania
 
Alisema kuwa muungano ukivunjika na  kufikia hatua ya mgawanyiko watambue kuwa hata  Unguja na Pemba navyo vitagawanyika kwa sababu leo wamedai hati ya Muungano wa Watanzania mwisho
watataka hati ya Unguja na Pemba lakini Wazazibar hawakubali msimamo wa serikali tatu.
 
Katika mbio hizo vijana hao walikabidhi kwa kaimu mkuu wa wilaya ya Iringa, Gerald Guninita picha ya Rais wa kwanza wa Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere na picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Shekhe Abeid Amani Karume pamoja na mabango mawili moja likiwa na ramani ya Tanzania na lingine likiwa na ujumbe maaulum wa mbio hizo unaosema, miaka 50 ya Muungano, “Dumisha Muungano vijana tutumie fursa zilizopo kwa maendeleo yetu, Tanzania kwanza mengine baadae.

MPIGA GITAA SKYLIGHT BAND CHIRI CHALLA AFARIKI GHAFLA

10173726_10152036323227864_1413106576404088176_n

Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.

Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali sehemu kichwani.

10268531_10152035773597864_7736400417218686840_n

Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.

Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.

Kwa mawasiliano zaidi namba ya Meneja wa Bendi +255 715 677 499.

MATUKIO BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

1 (18) Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo leo mjini Dodoma, kilichokuwa kikijadili mambo mbalimbali ikiwemo jinisi ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni.4 (7)Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba Pande Ameir Kificho akitoa mchango wake wakati wa kikao cha Kamati hiyo leo mjini Dodoma, kilichokuwa kikijadili mambo mbalimbali ikiwemo jinisi ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni.

6 (4)Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kushoto) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo  leo mjini Dodoma wakati wakijadili mambo mbalimbali ikiwemo jinisi ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni. Kulia ni Katibu wa Bunge hilo Yahya Khamis Hamad. 

Picha na Bunge Maalum la Katiba-Dodoma

RAIS DK.SHEIN AKIZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA KATIBA NA SHERIA

IMG_9916 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar jana jioni, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]IMG_9926Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya  Katiba na Sheria wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi kwa kipindi cha robo mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana jioni, chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9930Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria,katika kikao cha utekelezaji Mpango kazi kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini  Zanzibar jana jioni, [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Baraza Kuu la Wafanyakazi NSSF Lakutana Dar es Salaam

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Kulia ni Katibu wake.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa  Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano  wao.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (wa kwanza kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa shirika hilo, ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (katikati) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi waandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo.

BARAZA Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam tangu juzi kufanya vikao vyake vya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utendaji kazi, kupitia mikakati na malengo mbalimbali iliyojiwekea.

Mkutano huo ambao pia umejadili na kupitisha bajeti ya shirika kwa mwaka 2014/15 umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF uliopo Katika Jengo la shirika hilo ‘WeterFront House’ la jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umejumuisha Watendaji Wakuu toka Makao Makuu, Mameneja wa Mikoa, Watendaji wa kuu wa mikoa na wajumbe wengine wanaounda baraza la wafanyakazi la NSSF. Jumla ya wajumbe 142 wameshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili. Shirika la NSSF ni miongoni mwa mwashirika makubwa ya hifadhi ya jamii nchini yenye vitega uchumi lukuki na vya thamani kubwa vinaochangia kukua kwa uchumi wa taifa.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com