MWANAMUZIKI ROGERS LUCAS ATATISHA NA “RUDI”!!

Rogers Lucas akiwa katika picha ya pamoja na Gwiji la muziki kutoka Paraguay Ricardo Flencha mara baada ya onyesho lao nchini Uswisi.
Rogers katikati akipiga ngoma na kuimba wakati walipokuwa jukwaani katika moja ya matamasha yaliyofanyika ulaya hivi karibuni ambapo mwanamuziki huyo kutoka Tanzania alishiriki.

Kundi la wanamuziki walioshiriki na mwanamuziki Rogers Lucas katika tamasha la muziki nchini ujerumani wakiwa katika picha ya pamoja.

Mwanamuziki chipukizi Rogers Lucas yuko mbioni kuingiza Albam yake mpya sokoni baada ya kuikamilisha kwa mafanikio huku akipata mialiko kadhaa katika nchi za Magharibi kama Ujerumani Uswisi na Australia, Albam hiyo inajulikana kwa jina la Rudi ni moja ya Albam bora zilizowahi kutolewa na wanamuziki Chipukizi katika muziki wa BongoFleva hapa nchini .

Rogers kijana anayeonekana mtulivu anayependa kutembea huku akiwa amebeba gitaa lake amekuwa akipata mialiko kadhaa hapa nchini na nje ya nchi ambapo amefanya maonyesho yake kwa mafanikio makubwa, lakini pia ameshirikiana na wanamuziki wakubwa kama vile Ricardo Flecha kutoka Paraguay Amerika ya kusini mwanamuziki ambaye anaheshimika sana katika ukanda huo kwa uwezo wake katika kupiga muziki.

Wakati Fulani niliwahi kumshuhudia Rogers ambaye ana uwezo mkubwa katika kupiga gitaa na kuimba katika onyesho moja la mavazi lililohusisha wanamitindo maarufu hapa nchini ambalo lilifanyika kwenye Hoteli ya kitalii ya Kilimanjaro Kempiski katikati ya mwaka huu alionyesha uwezo mkubwa na sauti yake ilivutia watu wengi waliohudhuria katika Onyesho hilo.

Albam ya Rogers ina nyimbo nane ambazo ni Mama, Niambie Leo, Jasho la Upendo, Ni Wewe, Si Utani, Hayupo na Rudi wimbo uliobeba jina la Albam hiyo, mpaka sasa Albam iko tayari na itakuwa madukani hivi karibuni watu wote wakae mkao wa kula na kupata burudani iliyomo ndani ya Albam hiyo.
admin

Got something to say? Go for it!