LEO NILIPATA NAFASI YA KUHUDHURIA KATIKA IBADA YA MCHUNGAJI FLORIAN KATUNZI WA KANISA LA EAGT CITY CENTER!!

Mchungaji Frolian Katunzi wa Kanisa la EAGT CITY CENTER akiwapa waumini wake neno la mungu katika ibada takatifu iliyofanyika kwenye ukumbi wa VETA No 72 kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam ambako kumekuwa kukifanyika ibada kama hiyo kila siku ya jumapili, ambapo pia amekuwa akitoa huduma ya maombezi siku ya Jumamosi .

Nilipata nafasi ya kuhudhuria katika ibada hiyo na nilifurahia mahubiri kwani yalikuwa ni mazuri na yenye kusisimua, nilijua kwamba ni kweli mungu anaweza kwani nimevuka milima na mabonde mpaka siku ya leo, lakini mungu amekuwa akinipigania na kunilinda wakati wote namshukuru sana mungu kwa yote aliyonitendea kwenye maisha yangu na familia yangu.

Kulikuwa na Kwaya ya Tunduma Salvation Singers yenye albam yake nzuri inayoitwa Usihuzunike nao walitia fora katika ibada hiyo huku wakicheza na kuimba kwa furaha walidhihirisha kwamba kweli ni wana wa mungu na wapo kwa kazi ya kumsifu mungu.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Zakayo Murro akiimba katika ibada hiyo na kuwafanya baadhi ya waumini mwaliohudhuria katika ibada hiyo kushindwa kukaa kwenye viti wakiimba kwa furaha kubwa.

Zakayo alikuwa akiimba wimbo wake wa Nipatie Yesu aliourekodi katika Studio za Totoz zilizoko Sinza chini ya Peter Gunju ambapo anatarajia kutoa albam yake ya nyimbo nane yenye jina Nipatie Yesu.

Waumini mbalimbali wa kanisa la EAGT CITY CENTER wakisifu na kuabudu wakati wa ibada takatifu iliyofanyika kwenye ukumbi wa VETA 72 kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es vsalaam.
Waumini mbalimbali wa kanisa la EAGT CITY CENTER wakisifu na kuabudu wakati wa ibada takatifu iliyofanyika kwenye ukumbi wa VETA 72 kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es vsalaam.
admin

Got something to say? Go for it!