SAMWEL SITTA ATEMWA NA CCM KUGOMBEA USPIKA WA BUNGE !

Spika aliyemaliza muda wake Samuel Sitta akisalimiana na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma leo, katika kikao hicho mgombea aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililomaliza muda wake ambaye alikuwa anatetea kiti hicho ametemwa na kamati kuu ya chama cha Mapinduzi CCM na kumtema Samwel Sitta huku ikiwapitisha Anna Makinda, Anna Abdallah na Kate Kamba ambao watapigiwa kura na wajumbe wa Harmashauri kuu ya Chama Hicho na kupata jina moja litakalopelekwa mbele ya wabunge ili kupigiwa kura kwa ajili ya kupata mgombea wa uspika wa bunge hilo kupitia CCM amesema Makamba katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Yusuf Makamba.
(Picha na Freddy Maro wa Ikulu)
Spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano aliyemaliza muda wake Samuel Sitta akimpongeza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kwa kuchaguliwa tena kuendelea na wadhifa huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)
Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma leo mchana.Kutoka kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu SMZ Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu CCM Yusuf Makamba, Makamu wa CCM Bara, Pius Msekwa na Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein.
admin

Got something to say? Go for it!