MBEYA EXPRESS WANATISHA KWA MABASI BOMBA MBEYA-DAR

Katikati ni Rich Kulembeleka Rafiki yangu wa siku nyingi kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa Dereva wa Basi la kampuni mpya ya Mbeya Express, lianalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Mbeya, kulia ni Msaidizi wa dereva Makao Gahu, na kushoto ni fundi wa kampuni hiyo Daud Awadh wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya basi lao, wakati tulipofika maeneo ya Kitonga na kusimama kwa muda mfupi kwa ajili ya kupata Chakula.

Kampuni hii ni mpya na ina mabasi ya kisasa, tulisafiri vizuri na wafanyakzi wake ni wakarimu sana ukitaka kwenda mbeya na kurudi Dar es salaam unaweza kutumia usafiri huu kwani, ni usafiri bomba sana.
Hapa ilikuwa ni kitonga leo baada ya mvua kunyesha na lami kulowa maji pamlichafuka sana jambo lililofanya maroli mengi kushindwa kupanda na kusababisha foleni,kutokana na utelezi wa mafuta ya dizeli yanayomwagika kutoka kwenye matanki ya maroli yanayosafirisha mafuta, anayeonekana chini ni Makao Gahu msaidizi wa dereva wa basi hilo.
Hapa ni Starcom Kitonga Hotel tulisimama hapa kwa ajili ya mlo wa mchana kabla ya kuendelea na safari.
Mvua inapiga na maroli yanapanda kwa shida ktika mlima Kitonga na kutokana na mvua hiyo kulikuwa na foleni kubwa ya magari mchana wa leo.
Kama unavyoona basi la kampuni ya Abood likijaribu kupishana na maroli hayo, mabasi mengi yalichelewa ratiba yao ya kila siku.


admin

Got something to say? Go for it!