WASANII wa muziki wa kizazi kipya na dansi Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry Samir ‘Mr Blu’, wakiwa na kundi la Mapacha Watatu ambalo linaongozwa na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’, Junior Kalala ‘Kalala Junior’, na Joseph Michael ‘Jose Mara’, na kundi la muziki wa mwambao la Super Shine, usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Wanamuziki hao walivunja rekodi ya mashabiki wengi waliowahi kushuhudia makamuzi kama hayo katika kituo hicho cha burudani nchini.
Shoo hiyo pia ilisindikizwa na makundi mengine kama Wakali Dancers, na wasaniii wengine wa Bongo Fleva wakiwemo Zuhura na Dogo Mfaume na Hejos Band.
Watoto wakiserebuka ukumbini.
Watoto wakiserebuka ukumbini.








0 maoni:
Post a Comment