
Meneja wa kinwaji cha Serengeti Lager kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo anayeendesha gari pamoja na Kanji ambaye pia ni mfanyakazi wa kampuni hiyo wakiongoza msafara wakati ulipopita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo, kuutambulisha muonekano mpya wa nembo ya bia ya Serengeti Lager huku ikiwa na ubora na viwango vilevile.

Mkurugenzi wa FULLSHANGWE Bw. John Bukuku akisalimiana na Kamalade Ali Choki mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo na bendi yake ambaye ndiye anayetoa burudani katika promosheni hiyo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa FULLSHANGWE akipiga stori na maafande wa kikosi cha usalama barabarani wakati walipokutana katika shughuli za promosheni hiyo kwenye makutano ya barabara za Shauri Moyo na Uhuru.

Kamalade Ali Choki na mkundi lake la Extra Bongo wakifanya vitu vyao kwenye jukwaa la gari maalum.

Mpiga gitaa la bass wa Extra Bongo akipiga gitaa huku mnenguaji wa bendi hiyo akicheza mbele yake wakati msafara huo ulipopita katika barabara ya Uhuru leo.

Extra Bongo wacharuka na kumwaga mauno barabarani wakati msafara wa promosheni ya Muonekano Mpya wa Dhahabu ukiendelea katika mitaa mbalimbali jijini Dar es salaam leo.
Muonekano mpya wa Dhahabu wa Serengeti Lager akipita maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam
Msafara akupita katika maeneo ya BP katika baranbara ya Bandari ukitokea Chang'ombe Kiwandani na kuelekea maeneo ya Kariakoo jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Post a Comment