TUTUMIE HABARI NA PICHA MDAU!!

Friday, January 27, 2012

RC Arusha ataka katibu tawala kuitisha mkutano wa haraka kwa wananchi ambao wamenunua viwanja katika halmashauri ya Arusha vijijini

Na Gladness Mushi wa Fullshangwe- Arusha Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amemuagiza katibu tawala wa mkoa huo kuitisha cha haraka sana kikao pamoja na kamati za ugawaji wa viwanja vya halimashauri ya arusha vijijini ili waweze kutekeleza na kuweka maamuzi ya ahadi za wananchi walizowahidi mara walipouziwa viwanja na halimashauri hiyo.

Amefikia hatua hiyo baada ya Wananchi ambao waliuziwa viwanja na halmashauri ya Arusha vijijini katika eneo la Burka kuilalamikia halmashauri hiyo kwa kutoweka miundombinu na huduma muhimu za kijamii kwenye eneo hilo na hivyo kusababisha kero kwa wale wanaofanya shughuli za ujenzi na ambao wanataka kuhamia kwenye makazi hayo.

Mulongo alisema kuwa ni vema kikao kikaitishwa mara moja na kamati ikaamua kutekeleza ahadi zote ambazo waliwekeana na wateja wao pindi walipogawiana viwanja na kuwaidi kuwa watawawekea huduma muihimu na hadi sasa hawajawekewa hali inayoonekana kuwa hawajaatendewa haki.

Mbali na hayo mkuu huyo aliitaka halimashauri hiyo arusha vijijini kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu kwa wale wote waliogawiwa viwanja kuhakikisha kuwa wanachukua hati zao milki za ardhi kwa kuwa hadi sasa walionunua viwanja hivyo hawajachukua hati zao hali inayompelekea mkuu huyo kuwa na mashaka .

"Haiwezekani mtu aweze kununua kiwanja cha shilingi milioni kumi na ashindwe kufuatilia hati yake miliki la sivyo kutakuwa na sababu hivyo nawaombeni mfanye jitihada za kila namna kwa watu hawa walionunua viwanja waje wachukue hati zao "alisema Mulongo

Hata hivyo Mulongo akiwa kwenye ziara hiyo ya kutembelea viwanja hivyo vilivopo eneo la burka alishuhudia kutokuwepo kwa huduma hizo hata moja walizohidi kwa wananchi hao huku akiiisisitiza kuhakikisha kuwa barabara zifunguliwa mapema iwezekanavyo katika eneo hilo.

0 maoni: