TUTUMIE HABARI NA PICHA MDAU!!

Friday, January 27, 2012

HANCE KIMOLA, KIJANA WA KITANZANIA KUWAKILISHA KATIKA MCHEZO MAALUM WA TV WA GUINNESS (GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE CELEBRITY FINALE)

Karibu michezo 30,000 ilichezwa kupitia kwenye simu za mkononi Africa Mashariki kwenye mchezo wa simu ulioendana sambamba na kipindi maalum cha Guinness Football Challenge, kipindi kilichorushwa hewanina ITV.

Mchezo huo uliopo katika tovuti ya www.mguinessvip.com ni wa kuburudishana ulipata wapenzi wengi kabisa na kujipatia umaarufu nchini.

Bwana Hance Kimola,waubungo Dar es salaam nikijana wakitanzania aliyeibukana pointi nyingi kabisana hivyo kujipatia nafasi ya kushiriki katika kipindi maalum, GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE CLEBRITY FINALE, ambacho kitachezeshwa Afrika Kusini. Kijana Hance ameondoka asubuhi kwa ndege ya shirika la ndege laAfrika Kusini(South Africa Airways) kuelekea Afrika kusini.

Hii ni Fursa ya kipekee kwa kijana huyu ambaye atapewa mshiriki mwenza, kati ya wakongwe kwenye tasnia yasoka,wafuatao: Jay JayOkocha ,MarcelDesaily, Rigobert Song na KalushaBwalya. Hance aliibuka mshindi wa mchezo huu ambao unajulikana kwa wengi kama‘Guinness Mobigame’nchini Tanzania. Pia alipatikana mshindi mmoja kutoka nchi ya Kenya, Uganda, Ghana na Cameroon.

Katika kipindi hiki cha ‘GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE CELEBRITY FINALE’ Kila mmoja kati ya vijana hao,baada ya kupewa mshiriki mwenza awe Okocha, Desaily , Song au Kalusha, itabidi wacheze kwa umakini mkubwa ili waonyeshe ujuzi wao wa maarifa ya mpira.

Bwana Hance ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam pamoja na mshiriki mwenza watakuwa na nafasi ya kujinyakulia zawadi nono kama wakiibuka washindi.

Baada ya kupata taarifa kuhusu fursahii bwanaHance alisema “Mchezowa GUINNESS MOBI GAME ni mchezo mzuri sana, na hata kama nina ujuzi wa soka, nilijifunza mengi. Nilipendelea kucheza na rafiki zangu wakati wakutazama ‘English premier league, pia nilikuwa nafuatilia sana Guinness Football Challenge kupitia ITV. Kesho naelekea AfrikaKusini, passport naticketi tayari nimeshakabidhiwa na naishukuru sana kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji cha Guinness. Nasubiria kwa hamu kujua nani atakuwa mwenzangu na ningependa ‘partner’ wangu awe Okocha. Ila,hata nikipewa , Marcel, Song au Kalusha bado naamini nitafika ‘round’ya mwisho, na nitailetea heshima nchi yangu”.

Meneja wa GUINNESS katika kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Maurice Njowoka amesema “kipindi hiki cha GUINNESSFOOTBALL CHALLENGE kimekuwa na mafanikio makubwa,na kwa mara nyingine tena tumeweza kuwapa wapenzi wampira fursa ya kujaribu ujuzi wao kwenye mchezo maarufu wa simu za mkononi wa GUINNESS MOBI GAME.“

Kipindi hiki cha ‘GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE CLELEBRITY FINALE’ kinatayarishwanaEndemol, kampuni ya AfrikaKusini maarufu kwa kutengeneza vipindi mbalimbali.Kwa hapa nchini kitaonyeshwa nakituo cha Televisheni cha ITV.

0 maoni: