Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Kampeni ya usafi katika Manispaa ya Sumbawanga ijulikanayo kama "Sumbawanga Ng'ara". Kampeni hiyo ilianzishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa kwa nia ya kuufanya Mji huo uwe wa mfano na wa kupendeza. Kushoto kwake aliyeshikilia utepe ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Kampeni hiyo inaenda sambasamba na Kauli Mbiu ya "Dumisha Usafi wa Mazingira, Dumisha Upandaji Miti na Dumisha Miundombinu Daima".
Kwa hisani ya http://www.rukwareview.blogspot.com/
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikabidhi vifaa vya usafi kwa kikundi cha usafi cha Manispaa ya Sumbawanga kama sehemu ya Kampeni ya usafi wa Mazingira katika Mji wa Sumbawanga.
Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais akifagia katika moja ya barabara za lami katika Mji wa Sumbawanga kama ishara ya kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye usafi wa Mji huo.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la Msingi katika moja ya barabara kuu za Mji wa Sumbawanga sehemu aliyozindulia Kampeni ya usafi kwa Mji wa Sumbawanga. Kushoto ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.







0 maoni:
Post a Comment