TUTUMIE HABARI NA PICHA MDAU!!

Thursday, February 23, 2012

RDC CONGO vs TAIFA STARS : HAKUNA MBABE UWANJA WA TAIFA

Mchezaji Ilunga (kushoto)wa Jamhuri ya Kiodemokrasia ya Congo akichuana vikali na mchezaji Hussein Javu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars wakati wa mchezo wao wa kirafiki unaofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jioni hii. Mchezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya mapambano ya timu hizo kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini, ambapo Taifa Stars itakutana na Msumbiji na RDC Congo itakutana na Sychelies, mpaka mpira unamalizika hakuna timu iliyopata goli hivyo matokeo ya timu hizo mpaka mwisho yamekuwa 0-0 kwa timu zote.
Kocha wa timu ya Taifa Stars Jan Paulsen akimuelekeza jambo Aggrey Morris mchezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.
Wachezaji wa Timu ya RDC Congo na Taifa Stars wakisalimiana kabla ya mchezo huo kuanza kwenye uwanja wa taifa.

0 maoni: