Archive for August 2nd, 2012

RAIS KIKWETE ATOA KIFUTA JASHO CHA NG’OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji hicho cha Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Kikwete akiwa na Viongozi wengine Meza kuu.
Rais Kikwete akielekea kwenye Jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hafafika na kuigawa kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Mbonduli.
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa baada ya kufanyika kwa mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng’ombe kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng’ombe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika Mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka.
Mh. Lowassa na Mh. Lukuvi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na kina mama wa Kimasai katika kijiji cha Makuyuni leo.
Burudani kutoka kwa Vijana wa JKT.

RAIS KIKWETE ATOA KIFUTA JASHO CHA NG’OMBE KWA WANANCHI WA MONDULI

Rais  Jakaya Mrisho kikwete akizindua
mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za
Mkoa wa Arusha kama kifuta jashp cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000
kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009
(PICHA NA IKULU) 
 
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ng’ombe
mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na na ukame mwaka 2008/2009
ambapo walipoteza mifugo yao yote. Hafla hii imefanyika leo Monduli.
Picha na Ikulu.

 

SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500
kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha
kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari
zake mwaka 2008/2009.

Ahadi hiyo imetolewa leo, Alhamisi,
Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa
waliopotelewa mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika
Makuyuni wilayani humo.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na
viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo,
Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni
mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.

Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na
Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali
katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.

Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete
alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika
mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo

PINDA AZINDUA KITABU CHA WANASAYANSI 31 MABINGWA WA KITANZANIA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesha kitabu kiitwacho Lighting
Fire kilichoandikwa na wanasayansi 31 Mabingwa wa Kitanzania baada ya
kukizindua kwenye ukumbi wa Tume ya taifa ya Sayansi na Tekinolojia,
Kijitonyama jijini Dar es salaam Agosti 2, 2012. Kushoto ni  Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Profesa  Makame Mbalawa na Kulia ni
Rais wa Tanzania Academy of Science (TAAS), Profesa Esther Mwaikambo.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda akisalimiana  na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma,
Profesa, Idris Kikula baada  ya kuzindua  kitabu kiitwacho Lighting fire
kilichoandikwa na  wanasayansi 31 mabingwa wa kitanzania, kwenye ukumbi
wa Tume ya Taifa ya Sayansi  na Tekinoloji, Kijitonyama jijini Dar es
salaam Agosti 2, 2012. Kushoto ni Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu  Huria cha
Tanzania, Profesa  Tolly Mbwete. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AZINDUA SHULE YA URAFIKI

Na Salama Thalaba, ZJMMC
Makamu
wa Pili wa Rais Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd leo amezindua ujenzi wa
Skuli ya msingi iliyopewa jina la Urafiki inayofadhiliwa na Serikali ya
Jamhuri ya Watu wa China.
 
Balozi Seif Idd aliyasema hayo katika skuli ya Mwanakwerekwe C wakati akizindua ujenzi wa skuli ya urafiki inayofafdhiliwa  na Serikali ya China kwa Dola za Marekani 1.6.
katika
sherehe za uzinduzi wa Skuli hiyo yenye madarasa kumi na mbili,Makamu
wa Rais amesema kwamba wananchi wa Zanzibar wanathamini mchango
unaotolewa na Serikali ya China.
Pia
alisema Serikali inaupa kipaumbele sana mchango huo kwa kuchangia
katika sekta ya Elimu kwani bila ya elimu hakuna maendeleo.
Aidha,
Balozi Seif Idd amesema kwamba Serikali itachukua kila jitihada
kuhakikisha tatizo la vikalio linamalizika katika skuli zote za Unguju
na Pemba alisema.
 Utoaji wa madeksi hayo

Mbali
na ujenzi wa Skuli hiyo, pia Serikali ya China kupitia Jimbo la Sichuan
imetoa jumla ya madawati 480 kwa ajili ya Skuli mbalimbali za Unguja.
Kwa
upande wake, Balozi mdogo wa China Zanzibar, Chen Qiman alisema
Serikali ya China itaendelea kuisaidia Zanzibar katika nyanja
mbalimbali.
Ameipongeza
Serikali kwa juhudi inazochukuwa kutekeleza mipango yake mbalimbali ya
kuwalatea maendeleo wananchi wa Zanzibar akitoa mfano suala zima la
elimu.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali,Ali Juma Shamuhuna ameipongeza Serikali ya
China kwa msaada wao kwa Wizara ya elimu hasa ujenzi wa Skuli hiyo
pamoja na msaada wa madawati.

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

Mwingulu Mchemba (kulia) wa jimbo la Iramba Mashariki akibadishana hoja na Mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa  Bungeni Dodoma (Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO).
Maafisa wa Bunge wakifuatilia hoja mbalimbali  za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa Fedha 2012-2013.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan  (kulia) na Mbunge wa Muheza Hebert Mtangi wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
. (
Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Naibu Spika Job Ndugai (kushoto) akimsikilza Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela katika viwanja vya Bunge Dodoma,(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

UVCCM ZANZIBAR: WANANCHI HAWAJAFUNGWA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA

 
Na Khadija Khamis,MAELEZO Zanzibar 
    
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi umesema wananchi hawajafungika kutoa
mawazo yao katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba,lakini msimamo wa CCM ni
kubaki katika mfumo wa muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Mjini hapa Jana, Naibu Katibu
Mkuu wa UVCCM Zanzíbar, Jamal Kassim Ali alisema kimsingi wananchi wako
huru kutoa maoni yao kuhusu aina ya mfumo wa Muungano,lakini kwa
wanachama wa CCM ni lazima wafuate msimamo wa Chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema kwamba Umoja wake unaamini katika kulinda na
kuhifadhi umoja na mshikamano uliopo hivyo ni muhimu kwa wananchi
kutokubali kushawishiwa kuvunja Muungano.
“Katika
suala la Muungano, CCM imeweka wazi kuwa itaendeleza muundo wa Muungano
wa Serikali mbili kama inavyoelezwa katika ibara ya 221(a) ya Katiba ya
Chama cha Mapinduzi sisi hatuwezi kuikiuka katiba hiyo” Alisema Jamal.
Naibu
Katibu Mkuu huyo alisema Vijana wa CCM wanakubaliana na muongozo wa
Chama hicho hasa katika suala la Muungano wa Serikali mbili ikiwa
miongoni mwa mambo 15 ya msingi yaliyopendekezwa na Chama hicho kuwa
yawemo katika katiba mpya.

“Tunakubaliana
na suala la kuyatoa katika orodha ya mambo ya Muungano yale yote
yanayoikwaza Zanzíbar kiuchumi ikiwemo suala la mafuta na gesi asilia,
ushuru wa forodha, mikopo ya nje” Alisema Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM
Zanzíbar.
Jamal
alisema kuwa vijana wa CCM wanaamini kasoro zilizokuwepo katika
Muungano zinazungumzika na kurekebishika kwa hivyo hakuna haja wala
sababu ya watu kufanya fujo au kutumia matamshi ya jazba lililo muhimu
ni wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Jaji
Warioba ambayo tayari imeanza kazi ya kuchukua maoni.
Wakati
huo huo, Baraza la Wazee CCM kupitia Baraza lao la ushauri
wamesikitikishwa na baadhi ya vijana kufanya vitendo vya kuashiria
kuvunja amani na umoja wa nchi.
Katika
taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Baraza
hilo, Makame Mzee Suleiman, alisema wamechukizwa kuona baadhi ya
viongozi akiwemo Rais wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
wakitumia picha yake wakati akihutubia wanachama wa CCM kwa madhumuni
yasiyokuwa yake.
“Lakini
kama yote hayo hayatoshi kutukera sisi wazee tunalaani kwa kauli moja
walioeneza vipeperushi kumuhusisha Rais wetu mpendwa Dk. Ali Mohammed
Shein juu ya suala zima la kuridhia Muungano wa mkataba” Alisema
Mwenyekiti Makame Mzee.
Katika
taarifa hiyo Baraza la Wazee walisema kwamba katika vipeperushi hivyo
anaonekana Rais Dk Shein akiwaelezea mamia ya wana CCM jambo hilo
halikuwa la kweli na wamewataka wanaharakati waseme yao wasiwasemee
viongozi wala wnanchi.
Baraza
hilo limeshauri wananchi waachwe kuingia kwenye mchakato wa katiba
watoe maoni yao juu ya katiba ili hatimaye Tanzania ifikie katika lengo
lililokusudiwa la kupata katiba mpya.

DK KIGODA AITAKA TBS KUFANYA UKAGUZI WA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI

WAZIRI
wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda amelitaka Shirika la Viwango (TBS),
kuhakikisha linafanya ukaguzi wa bidhaa kutoka nje kabla hazijaingizwa nchini
ili kuepukana na tabia nchi hii kugeuzwa dampo la bidhaa hafifu.

Kauli
hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana, wakati alipokuwa akizindua Ofisi ndogo
ya shirika hilo, inayoshughulika na ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Dk
Kigoda alisema iwapo shirika hilo litafanikiwa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa
hafifu nchini anaamini kelele zote zinazopigwa kuwa wao ndio chanzo cha
uingizwaji wa biadhaa hizo zitakwisha.
“Nawaagiza
TBS kupitia madukani na sokoni ili kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ubora wa
bidhaa na zile bidhaa mtakazokuta ni hafifu, zitoweni na kuziharibu na hao
wafanyabishara watozwe faini za kuharibu bidhaa zao”alisema Dk Kigoda.
Alibainisha
kuwa Wizara yake inatarajia kupata taarifa juu ya utekelezaji wa maagizo hayo
kwa vipindi vya kila robo mwaka ili kujua utaratibu wa utekelezaji.
Akifafanua
madhumuni ya wizara ni kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kama vile
Mamlaka ya Mapato (TRA) Baraza  
la Mazingira ,Mamlaka ya Chakula na Madawa (TFDA), Mkemia Mkuu wa  serikali, pamoja na  Tume ya Ushindani  ili kuhakikisha bidhaa za nje zinapimwa
maridhawa.
“Ili
shehena za bidhaa hafifu zizibitiwe kuingia sokoni na kurudishwa zilikotoka”
kwa mujibu Dk Kigoda.
Naye
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi 
ya shirika hilo, Oliver Mhaiki   alitabanaisha kwamba uzinduzi wa ofisi hiyo ni
muendelezo wa jitihada za shirika kusogeza huduma kwa wateja.
Vile
vile alifafanua kuwa TBS 
imeshapanua wigo kwa kufungua ofisi katika maeneo mbalimbali kama vile
Sirari, Holili, Horohoro, Bandari ya Tanga sanjari na Namanga mkoani Arusha,
kwa lengo la kuwasogezea huduma wadau na kuwapunguzia adha katiaka shughuli zao
za kibiashara.

 


RAMBIRAMBI MSIBA WA MSAFIRI MKEREMI

 
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Msafiri Mkeremi kilichotokea leo
alfajiri (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Urambo
mkoani Tabora.
Licha
ya kuwa mwamuzi, Mkeremi aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF kwa vipindi viwili
tofauti. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT).
 
Vilevile
aliwahi kuwa mkufunzi wa waamuzi, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa
wa Pwani.
 
Kwa
upande wa vyama vya mpira wa miguu aliwahi kuwa kiongozi katika mikoa
ya Tabora, Pwani na wilayani Mpanda katika Mkoa wa Rukwa.
 
Msiba
wa Mkeremi uko nyumbani kwake Urambo, na kwa mujibu wa mtoto wake
Masoud Mkeremi, atazikwa Jumamosi kwenye makaburi ya Msafa yaliyoko
wilayani Urambo.
 
TFF
inatoa pole kwa familia na kuitaka kuwa na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu
kama rambirambi zake.
 
Marehemu aliyekuwa akisumbuliwa na presha na ugonjwa wa kisukari ameacha wajane wawili na watoto 12.  Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina

EXTRA BONGO WAFANYA KWELI FINLAND

  Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ali Choki kulia akikamua pamoja na wanamuziki wa bendi hiyo  jijini kwenye ukumbi wa Tampere jijini Finland, bendi hiyo iko nchini Finland kwa maonyesho kadhaa ya kimuziki na kujitangaza katika anga za kimataifa kuutangaza muziki wa wa Tanzania.

Mahojiano na Aminiel Johnson Mzava.


Mahojiano na Aminiel Johnson Mzava. Pauline Johnson Mzava na Pastor Faye Chandler Washington DC wakiongelea uvumbuzi wa nyimbo za Injili.

Pauline Johnson Mzava (Kushoto) pamoja na Pastor Faye Pastor Faye Chandler, wakiimba nyimbo za injili ndani ya studio yao iliopo Washington DC.

Johnson Mzava akipata picha ya pamoja na mdhamini wa pendolake katikati pamoja na Pastor Faye Pastor Faye Chandler, wa kwanza kushoto pamoja na dogo Barack Johnson Mzava aliebebwa!

Johnson Mzava almarifu Aminiel, akizungumzia historia yake kwa ufupi, pamoja na uzinduzi wa Album ya nyimbo za Injili wakiwa pamoja na mdhamini wa pendo lake Pauline Johnson Mzava pamoja na pastor Faye Chandler jiji Washington DC Nchini Marekani (Picha na http://swahilivilla.blogspot.com/)

Airtel donates books to Kisawasawa secondary school in Kilombero Morogoro


Airtel Tanzania has today donated education books to Kisawasawa


secondary school been part of its corporate social responsibility


activity aiming to support the education sector under its Shule Yetu


project.


The handover ceremony of the books worth 2million shilling was held at


Kisawasawa Secondary school and was attended by the members of press,


Kisawasawa representatives and Airtel staffs.


Speaking during the handover ceremony Airtel Public Relations and


Events Officer Dangio Kaniki   said “We understand the shortage of


teaching aids in most of the schools in the country; this is why we


are committed to support the government under ministry of education to


ensure we contribute to the education sector in the country. We


recognize education has the fundamental role and is key to the


economic development, poverty alleviation, and is the basis for future


manpower/ employee that provides great leaders to our nation. This is


a continuation of our Shule Yetu programme that has been in existence


for over 6 years”.


“We are highly committed towards supporting Tanzanian communities not


only by providing communications services but also by improving the


education level in the country; we applaud the government efforts but


realize that we also have a role to play, which brings us to Kisawaswa


today. Airtel Tanzania has given equal opportunity to schools from all


regions in the country including the aisles to ensure the educational


support reaches most of the students and reduce the need for


educational and scholastic materials. Today we continue demonstrating


our commitment by this books donation to Kisawasawa Secondary school


in Kilombero Morogoro and believe it will be significant to Kisawasawa


students and teachers”. said Kaniki.


On his part Kisawasawa head teacher Munesi A Msigwa expressed his


appreciation towards the books donation and assured Airtel and the


community members in Morogoro that Airtel support will be kept to good


use and ensures the education level at Kisawaswa is promoted. He


added,”Airtel donation is true demonstrations of corporate willingness


to support the government in the education sector.We believe this


contribution will bring significant changes and increase our books


ratio from where it was. I urge and appeal to our students to make use


of the books donated by Airtel today to better their performance”.


Last week Airtel donated books to Mtipwa Seconday School in Singida,


in their urge to help more schools under the Shule Yetu project Airtel


will continue with its plan to reach more schools across the country


and provide sustainable support. Since the beginning of the project,


we have been able to support, approximately more than 1,000 secondary


and primary schools with teaching aid and scholastic materials across

the country.

WASHINDI SABA WAKABIDHIWA ZAWADI ZA SBL

Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo
(kushoto) akimpongeza mshindi wa pikipiki zilizokuwa zikishindaniwa katika
promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya
bia ya Serengeti  Bi Rahma  Rashid Ally aliye juu ya pikipiki yake
baada ya kukabidhiwa na meneja huyo. Wengine ni wafanyakazi na wawakilishi wa
kampunin ya bia ya Serengeti.


Meneja wa bia ya Serengeti bw Allan Chonjo
kulia akimpongeza bw.Joseph Felix aliye juu ya pikipiki yake baada ya
kukabidhiwa na meneja huyo. Wengine ni wafanya kazi wa kampuni ya bia Serengeti
.

Picha namba 8 ni meneja huyo akiwa na wafanya kazi wenzake
wakiwa katika picha ya pamoja na washindi 7 waliokabidhiwa zawadi zao jana
jijini Dar.


Kampuni ya bia ya Serengeti jana ilikabidhi
zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na
kampuni hiyo ijulikanayo kama ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL’
ambapo jana ilifikia tamati kwa kuchezesha droo ya mwisho na kuwapata
washindi wa gari moja , bajaj, moja na pikipiki na genereta .

Zawadi zilizokabidhiwa jana jioni ni pamoja na pikipiki mbili na jenereta tano zilizokabidhiwa kwa washindi wa jijini hapa na meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo .
Awali
akikabidhi zawadi hizo, meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo 
amesema promosheni hiyo imefika tamati na kwamba watanzania wajipange
upya kwani kuisha kwa promosheni hiyo ni mwanzo wa maandalizi ya
promosheni zingine. “ leo tumefunga rasmi promosheni yetu ya VUMBUA
HAZINA CHINI YA KIZIBO’ lakini bado tuna baadhi ya washindi ambao bado
hawajapewa zawadi zao kutokana na taratibu za usajili lakini siku chache
zijazo nao watakabidhiwa zawadio, sambamba na hilo napenda kutoa
shukrani zangu za dhati kabisa kwa niaba ya kampuni ya bia ya Serengeti
kwa wateja wetu juu ya ushirikiano mkubwa waliouonesha kwetu katika
kipindi chote cha promosheni yetu” alisema Chonjo.
Kwaupande
wao washindi waliokabidhiwa zawadi zao, waliipongeza sana kampuni ya
bia ya Serengeti kwa kujitolea kwake kushiriki katika shughuli
mbalimbali za kijamii
na kuisadia kwa njia mbalimbali kama ambavyo imetumia mamilioni ya
shilingi kuendesha promosheni kuwa kuliko yote kutokea hapa nchini. “
mimi naishukuru sana sbl kwani promosheni hii sasa imeweza kunitoa
katika hali mbaya ya kimaisha na kubadilisha kabisa maisha yangu”
aliseama mmoja wa washindi hao ambaye yeye amejishindia pikipiki mpya
kabisa.
Kampuni
ya bia ya Serengeti kupitia vinywaji vyake aina ya Serengeti Premium
Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager inaendesha promosheni  ya “ VUMBUA
HAZINA CHINI YA KIZIBO’, nchi nzima kwa muda  wa miezi minne na Promosheni hiyo imeweza kuleta mabadiliko yakinifu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
Serengeti Breweries Limited ni kampuni tanzu ya EABL/ DIAGEO.

HakiElimu waishauri Serikali, CWT kuhusu mgomo wa Walimu

Na Joachim Mushi, Thehabari.com
 
TAASISI ya HakiElimu nchini imeishauri Serikali pamoja na Chama Cha
Walimu Tanzania (CWT) kufikia makubaliano haraka iwezekanavyo, ili
kumaliza mgomo uliopo kwani waathirika zaidi na mgomo huo si wao bali ni
ni wanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mgomo wa walimu
unaoendelea maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kila mwanafunzi ana haki ya kujifunza na kuelimishwa, kitu
ambacho hawakipati kwa sasa kutokana na mgomo wa walimu wanaoshinikiza
Serikali iwaongeze mishahara pamoja na kuwaboreshea mazingira ya kazi
zao.
Mkurugenzi huyo alisema kauli ya Serikali kudai haina uwezo wa
kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya  watumishi wake haileti unafuu
wa maisha kwa watumishi wa umma hivyo kushauri iangalie namna ya
kufanya kumaliza mgogoro huo.
“HakiElimu inasisitiza kwamba nchi itafanikiwa kuboresha elimu
endapo tu itawekeza kwa walimu kwa kuboresha mazingira ya kazi, maslahi
ya walimu, kuwashirikisha walimu katika maamuzi kuhusu masuala ya elimu 
na kuwapa walimu mafunzo kazini. Elimu bora haiwezi kuletwa na walimu
walio hoi,” alisema Missokia.
Aidha amewataka walimu kuhakikisha wanadai haki zao huku
wakiendelea kuwajibika kwa kufundisha na kuendeleza elimu yetu, kwani
wanamgogoro na Serikali na wala si wanafunzi na jamii kwa ujumla.
 
“HakiElimu inawakumbusha walimu kuwajibika. Wadai haki zao, huku
wakitimiza wajibu wao wa kufundisha na kuendeleza elimu yetu. Wafundishe
kwa bidii bila kinyongo, kwa kuwa wasipowajibika watakuwa wanawaumiza
wanafunzi na jamii kwa ujumla. Mgogoro uliopo ni baina yao na Serikali,
na si wanafunzi,” alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji.
“Viongozi wa Serikali wasiwabeze walimu; kwa kufanya hivyo wanawakatisha
tamaa. Hata kama baadhi ya walimu hawakusoma kwa miaka mingi kama
ilivyo kwa fani nyingine, wana umuhimu mkubwa sana. Ndio wanaowaandaa
watanzania wa leo na kesho kimtazamo na kimaarifa. Hivyo, kudai
kuboreshewa mazingira ya kazi ni haki yao; na Serikali inaweza kutimiza
wajibu wake kwa kuwasikiliza na kushauriana nao bila ubabe na kejeli,”
alisema.
Pamoja na hayo ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuingilia kati mgogoro huo na kutenga muda kujadili suala hilo kwa kina
ikiwa ni pamoja na kuishauri serikali, hasa kuhusu tahadhari za kuchukua
ili tatizo kama hili lisitokee tena.
“Bunge lina wajibu wa kuishauri na kuisimamia Serikali kuhusu sera,
utendaji na usimamizi wa elimu nchini. Inasikitisha kwamba Bunge
linakwepa kujadili tatizo hili kwa maelezo kwamba liko mahakamani.
Tunaamini kwamba mahakama italiangalia suala hili na kutenda haki,
lakini wajibu wa Bunge uko pale pale…” alisema Bi. Missokia.
Amekiri kwamba ni kweli gharama za maisha zinazidi kupanda, huku
mfumuko wa bei nao unaendelea kuwaumiza watumishi kila siku, hivyo
kuishauri Serikali kutafuta vyanzo mbadala vya mapato ili kuweza
kuwaboreshea mapato watumishi wake.
“Serikali ijijengee utaratibu wa kuboresha mazingira ya watumishi
wake, na si kusubiri kwenda mahakamani kuzuia watumishi kugoma.
Watumishi wa umma watafanya kazi kwa ari endapo tu wameridhika na
mazingira ya kazi na maslahi yao; na si kwa kutumia uamuzi wa mahakama
peke yake.”
Habari hii imeandaliwa na Mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)

NHIF, TAMISEMI, WIZARA YA AFYA ZAJADILI HUDUMA KWA WANACHAMA

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Emanuel Humba akitoa
maelezo ya utangulizi katika mkutano huo, kulia ni Naibu Katibu Mkuu
TAMISEMI, Jumanne Sagini
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi akitoa maelekezo kwa watendaji, kulia ni Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia.

Mawaziri wakifuatilia kwa karibu maelezo ya maofisa kutoka mfuko wa bima wa Afya NHIF wakati wa kujadilia huduma za wanachama wa mfuko huo mjini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

UBORESHAJI wa huduma za matibabu kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya hususan upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma ni
moja ya mambo yaliyojadiliwa mwishoni mwa wiki katika kikao kazi
kilichojumuisha wataalam kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na TAMISEMI.




Katika kikao kazi hicho ambacho kilihudhuriwa na maofisa wa ngazi za juu
katika taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
pamoja na TAMISEMI wakiwemo mawaziri wa pande zote mbili, walijadili kwa
kina namna ya kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la dawa ambalo
wanachama na wananchi kwa ujumla wanakutana nalo wakati wa kupata huduma
za matibabu.




Kwa upande wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kupitia Mkurugenzi wake
Mkuu, Emanuel Humba alisema kuwa Mfuko utaendelea na uboreshaji wa
huduma za matibabu kupitia mpango wa Mfuko huo wa mikopo ya vifaa tiba
na ukarabati wa majengo kwa vituo vilivyosajiliwa na Mfuko huo lakini
pia kuendelea kusajili maduka ya dawa muhimu ili wanachama wapate huduma
inayotakiwa na wananchi waone umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya wa
Jamii (CHF).




Aidha kwa upande wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao ndio wana jukumu la
usambazaji dawa, kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Joseph Mgaya, alisema kuwa
wanaendelea kushughulikia changamoto zilizopo kama kutokuwepo kwa
maoteo sahihi ya dawa ili hatimaye idara hiyo iweze kuondokana na
malalamiko yanayoelekezwa kwake.




Wakihitimisha kikao kazi hicho, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii pamoja
na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Hawa Ghasia, walizitaka
pande zote mbili kuhakikisha zinatekeleza maafikiano yaliyofikiwa katika
kikao hicho ili kipa upande uweze kutoa huduma nzuri kwa wananchi wa
Tanzania.




Aidha walisema kuwa njia pekee ya kuwakomboa wananchi au kuwafanya wawe
na uhakika wa kupata matibabu ni kuwahamasisha kujiunga na Mfuko wa Afya
wa Jamii (CHF) hivyo wakaitaka NHIF kuhakikisha inaongeza kasi ya
uelimishaji huku Serikali ikiendelea na uboreshaji wa huduma za matibabu
kwa kushirikiana na wadau wote wa sekta ya afya.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE MJINI MOROGORO

 Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua mkungu wa ndizi katika maonyesho ya
wakulima Nanenane Mjini Morogoro Agosti Mosi 2012. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafuta ya mawese yaliyokamuliwa
katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Ruvu wakati alipotembelea
Banda la Jeshi hilo kwenye  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini
Morogoro Agosti Mosi, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mzinga wa asili wa nyuki wadogo
wakati alipotembelea banda la Magereza kwenye maonyesho ya Wakulima
Nanenane Mjini Morogo Agosti Mosi, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

REDDS MISS MWANZA 2012/13 KUFANYIKA AGOSTI 31

Mrembo
wa mkoa wa Mwanza 2012/13 atapatikana ijumaa ya agosti 31 katika viwanja vya
Yatch Club Mwanza.

Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na muaandaji wa kampuni ya Sisi Entertainment
John Doto, amesema shindano hilo
linalovuta hisia za wengi ndani ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,
litashirikisha warembo tariban 20 kutoka wilaya zote za mkoa Mwanza.

John
Doto amesema warembo wote watakaa kambini kwa wiki mbili, ambapo kambi rasmi itaanza
tarehe 20 agosti mwaka huu katika hoteli ya Isamilo Lodge.
Shindano
la Redds Miss Mwanza 2012/13, lilisogezwa mbele kufuatia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wakiwa
kambini warembo watapata fursa ya kujifunza Mitembeo, Tabasamu, ufahamu wa
kujieleza pamoja na kuvumbua vipaji mbalimbali.

John
Dotto pia amesema warembo watakua na ziara ya kwenda kwenye mbuga za wanyama Serengeti,
kutoa misaada kwa watoto yatima, vikongwe pamoja na kufanya usafi kwenye moja
ya Hospitali Jijini Mwanza na moja ya barabara za Mwanza.

Kwa
miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Mwanza umekua ukitoa warembo wanaofanya vizuri
mashindano ya Taifa.

Itakumbukwa
Mwaka 2008 Nasreem Karim na Mwaka 2009 Miriam Gerald waliweza kushika Mataji ya
Miss Tanzania
wakitokea mkoa Mwanza.

HASSAN MOYO ATAKA WAZANZIBARI KUZUNGUMZIA MUSTAKABALI WA NCHI KWAKUWA NI MALI YAO

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar  
Mwanasiasa Mkongwe  Hassan Nassor  Moyo amewataka wananchi wa Zanzíbar  kuzungumzia suala zima la mustakbali wa  nchi  na  sio kuchanganya mambo   kwani nchi ni mali ya wananchi hivyo wanahaki ya kusikilizwa nini  wanataka.
Amesema  chama  kinaweza kuwepo na kuondoka lakini  nchi haiondoki hivyo wananchi wapewe fursa ya kuzungumzia  suala la nchi yao  na mambo wanayotaka kubadilishwa katika Muungano 
bila ya ugomvi wala fujo .
Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa Rumaisa  karibú na Hoteli ya Bwawani  wakati akizungumza  na waandishi wa habari wa vyombo  Mbali Mbali , wanafunzi wa chuo kikuu,pamoja  na wananchi waliofika hapo .
“Siwezi kupinga Muungano hata mara moja lakini Muungano tuubadilishe,” alisema, Moyo .
Aidha alisema  ili kuimarishwa  Muungano  ni lazima ufanyiwe marekebisho  ya kasoro  zinazojitokeza zirekebishwe kwa furaha na  sio kwa chuki na jazba .
“Tuzungumzie muungano kwanza katiba mwisho , tunataka uhuru wa kujitawala wenyewe sio kutawaliwa,”alisema Moyo.
Alidai kuwa wananchi   wengi wanasema hawautaki Muungano uliopo hivi sasa wanataka muungano ambao utaendana na wakati uliopo.
Aidha alifahamisha kwamba kuna baadhi ya  kasoro ambazo zilijitokeza  kabla ya Marehemu Karume ziliambiwa kwamba kurekebishwa bado haijafika wakati wake sasa wakati  ndio huu  wakurekebisha kasoro hizo.
Hassan Nassor Moyo ambaye anatokea katika vyama vya Wafanyakazi Zanzíbar  alishika nyadhifa  Mbale Mbale katika Serikali ya Mapinduzi na ya Jamhuri ya  Muungano  wa Tanzania.

HEPI BESDEI YA KUZALIWA SELLAH MUHIDIN

 Hepi Besdei ya Kuzaliwa mtoto Sellah Muhidin naye akaamua akasherehekee na wanafunzi wenzie wa shule ya Lady Chesam 
Nursery School iliyopo Oysterbay jijini Dar es salaam. Sellah, ambaye anatimiza miaka 3,  ni mtoto wa mwisho wa Ankal
Ankal Michuzi akipiga picha na mtoto wake Sellah  katikati na marafiki zake wakati wa besdei yake huko Oysterbay jijini Dar es salaam.