Archive for August 13th, 2012
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi ombeni Sefue afuturu na Viongozi waandimizi serikalini pamojana marais Wastaafu
Rais Mstaafu awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati
alipokuwa katika mazungumzo na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu
awamu ya Tatu Mhe. Benjamim William Mkapa(kushoto),Jaji Mkuu Othman
Chande(wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadik Meck
Sadik(watatu kushoto) pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue
jana jioni wakati wa futari iliyoandaliwa nyumbani kwa Balozi Sefue
jijini Dar es Salaam kwaajili ya viongozi mbalimbali serikalini.(picha
na Freddy Maro).

SIKU YA TAIFA LA TANZANIA YATIA FORA MAONYESHO YA EXPO KOREA
Sehemu
ndogo tu ya umati wa watu kutoka mataifa mbalimbali wakisikiliza hotuba
ya Waziri wa Biashara na Viwanda Mh. Dakta Abdallah Kigoda (hayupo pichani)
na kutazama burudani ya ngoma kutoka kikundi cha ngoma cha Bagamoyo
(TASUBA) katika ukumbi wa mikutano wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara
ya Korea (Korea Expo) yanayofanyika jijini Yeosu nchini Korea Kusini.

Kikundi
cha ngoma cha Chuo cha Sanaa cha Bagamoyo( TASUBA) kikitoa burudani
ya ngoma ya makabila ya mwambao wa pwani katika Banda la Tanzania kwenye
maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Korea mjini Yeosu Korea Kusini
katika siku ya Taifa la Tanzania.

Na
Geofrey Tengeneza –Yeosu Korea Kusini
Siku yaTaifa la Tanzania
katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Korea yanayofanyia katika
jiji la Yeosu hapa Korea iliyofanyika tarehe 8/8/2012 iliweka historia
na kuvutia maelfu ya wananchi wa Korea na watu mbalimbali kutoka mataifa
mengine wanaoshiriki katika maonesho haya ikilinganishwa na siku mataifa
mengi hususan kutoka barani Afrika.

Siku ya Tanzania ilianza
kwa maandamano ya watanzania wanoshiriki maonesho hayo sambamba na wale
wanoishi hapa mjini Yeosu yakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara
Mh. Dkt. Abdallah Kigoda yakianzia katika eneo maalumu la VIP ililo
karibu na geti kuu la kuingilia katika viwanja vya maonesho hayo majira
ya saa nne asubuhi yakipambwa kwa bendera ndogo zilizokuwa zikipungwa
hewani na watanzania hao wakiongozwa ngoma ya Ngongoti iliyokuwa
ikichezwa na kikundi cha ngoma kutoka Chuo cha Taifa cha Bagamoyo (TASUBA)
huku maandamo hayo yakishangiliwa na maelfu ya wananchi wa Korea.

Hali ilikuwa ni tete
zaidi katika ukumbi wa mikutano wa Maonesho hayo (Expo hall) ambapo
maelfu ya wananchi wa Korea walianza kujikusanya mapema kabisa kuanzia
saa 3.00 asubuhi kwa lengo ;la kuingia katika ukumbi ambao maandamano
yangefikia huku wakigombea maelfu ya bendera ndogo , DVDs na vipeperushi
mbalimbali vinavyoelezea utalii wa Tanzania vilivyokuwa vikitolewa na
maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) , Shirika la Hifadhi za Taifa
la Tanzania (TANAPA) na mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA).
Maafisa wa usalama wa Korea katika maonesho hayo walilazimika kufanya
kazi ya ziada kuzuia watu zaidi kuendelea kuingia katika ukumbi huo
ambakopia kikundi cha ngoma cha TASUBA kiliendela kulishambulia
jukwaa kwa mirindimo kambambe ya ngomaza aina mbalimbali za makabila
kutoka mwambao wa pwani wa Tanzania kabla na baada ya hotuba kutoka
kwa mgeni rasmi Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dkt. Abdallah Kigoda.

Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi mmoja wa raia wa Korea anayeshiriki maonesho haya katika
banda la Korea aliyetambulisha kwa jina la Yan Ching amesema amekuwa
katika maonesho haya toka yalipoanza mwezi wa tano na kushuhudia siku
za mataifa mbalimbali lakini hajapata kuona siku ya Taifa miongoni wa
mataifa ya Afrika iliyofana na kuvutia watu wengi sana kama hii ya
Tanzania. “Siku ya Taifa la Tanzania imetia fora sana unapolinganisha
na siku za mataifa mengine ya Afrika na hata baadhi ya mataifa yaliyoendelea
kutoka mabara mengine. Hii inaonyesha jinsi gani Tanzania inavyokubalika
kwa Wakorea pamoja na bidhaa zake mbalimbali wanazozionesha vikiwemo
vivutio vyenu vizuri vya utalii mnavyo vionesha katika maonesho
haya ya Expo” anasema Bwana Ching.

Katika siku hiyo ya
Taifa la Tanzania Waziri wa Biashara na Viwanda Mh. Dkt Abadallah Kigoda
pamoja na kutembelea mabanda kadhaa ya nchi za Kiafrika kama vile Kenya,
Uganda Rwanda na Angola, alipata pia fursa ya kutazama video maalumu
ya maliasili ya bahari na shughuli za baharini katika maneo pwani ya
Tanzania na Zanzibar iliyorushwa kwa takribani dakika 15 juu ya paa
katika eneo maarufu la wazi lililotengenezwa kwa utaalamu na teknolojia
ya hali juu kabisa linalovutia maelfu ya watu wanaoingia katika maonesho
haya.

Siku hii ya Taifa la
Tanzania ilihitimishwa na tafrija ya chakula cha jioni na kuhudhuriwa
na watanzania na waalikwa kutoka mataifa takribani yote yanayoshiriki
maonesho haya huku waalikwa wakiburudika vinywaji vya bia za Serengeti,
Kilimanjaro, Ndovu na Konyagi kutoka Tanzania sambamba na burudani maridhawa
ya ngoma za asili kutoka Tanzania iliyokuwa ikporomoshwa na kikundii
cha TASUBA kutoka Bagamoyo. Zaidi ya nchi 120 kutoka kote duniani zinashiriki
maonesho haya yaliyoanza tarehe 12/ 5/2012 na yanatarajiwa kumalizika
leo tarehe 13/08/2012.

UN YAWAKUTANISHA VIJANA NCHINI NA KUWATAKA KUJITAMBUA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA VIJANA DUNIANI
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel (katikati) kwa niaba ya Waziri Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara katika meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Vijana Kimataifa Duniani ambapo Tanzania iliadhimishwa katika viwanja vya Temeke Mwembeyanga. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Bw. Festus Ilako.
Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan (kushoto) akisalimia umati wa wakazi wa jijini Dar (hawapo pichani) na kutoa ujumbe kwa vijana kuungana na kujiepusha na mangonjwa hatarishi. Kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Bi. Mariam Khan.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Dkt. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha ujumbe kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo ambapo amewataka vijana kujitambua na kuwa na mikakati endelevu na kukaa kama vikundi ili Serikali iweze kuwasaidia kupata misaada na kuwawezesha kuwa na maendeleo endelevu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 11 Agosti na kutimiza malengo aliyokuwa akiyatafakari baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere juu ya Vijana.
Umati wa wakazi wa Temeke katika tamasha la siku ya maadhimisho ya Kimataifa ya Vijana Duniani ambako zilifanyika shughuli mbambali ikiwemo Ujumbe kutoka Serikalini na Kupima virusi vya Ukimwi bure.
Baadhi ya Vijana wakitazama machapisho ya vijarida mbalimbali vinavyotoa taarifa kuhusiana na Afya zao na jinsi ya kupata huduma.
Mmoja wa wakazi wa jijini Dar es Salaam akicheki Afya yake.
Wakazi waliohamasika kupima VVU na magonjwa ya Zinaa wakiwa katika foleni ya kupata huduma hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya vijana Duniani katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar.
Kikundi cha Sarakasi cha Rayon Kids kutoka Temeke kikitoa burudani wakati wa maadhimisho hayo.
Mheshimiwa mgeni rasmi hapa akikagua timu ya Mburahati Queens.
Pichani Juu na Chini Kipute kati ya Mburahati Queens na Evergreen Queens ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Evergreen kushinda 2-1.
Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake
Na Mwandishi Wetu Kambi ya Ilala
BONDIA wa Kike Lulu Kayage yupo katika mazoezi mazito
katika kambi ya ngumi ya Ilala Inayongozwa na Kocha Mkongwe Habibu
Kinyogoli ‘Masta’ na Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Nchini
Rajabu Mhamila ‘Super D’

Akizungumzia mchezo wa masumbwi ulivyomvutia mpaka
kuanza mazoezi katika kambi hiyo alisema anaupenda na pia
unamjenga kiafya na kimwili kwani amekuwa akishiriki mazoezi tangia
mwezi Aprili mwaka huu na maendeleo yake ni mazuri akiwa chini ya
uangalizi wa makocha wake hao
Bondia huyo wa kike aliyezaliwa 1990 ana matarajio makubwa ya kuwa bingwa wa dunia katika masumbwi hususani upande wa wanawake
Bondia
huyo anayevutiwa na uchezaji wa mkongwe wa masumbwi nchini Rashidi
Matumla ‘Snake Man’ anasema pia anavutiwa na bondia ambaye ni Mbunge wa Filpino Manny Paquaio
Katika mazoezi anayofanya na kambi ya Ilala ambayo wanawake wapo
wawili anaendelea kujisikia faraja kwa kuwa wapo katika mazoezi
pamoja kama ndugu na kuna nidhamu ya hali ya juu katika kambi
hiyo
Amewataka wanawake wajitokeze katika
mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo kama michezo mingine ambapo hata
ukiangalia mchezo huo mabondia wakimaliza mchezo wanakubatiana kwa furaha
ni kwa ajili ya kutambua kuwa mchezo wa masumbwi si uadui bali ni mchezo kama ilivyo michezo mingine
Vikwazo ambavyo amewahi kukutana navyo
ni pamoja na kukatishwa tamaa kwa watu ambao hawapendi michezo huo, kwani
wanasema mwanamke mzima unacheza ngumi huogopi kutolewa manundu kuharibiwa
sura. ehee uzuri wote huo! hayo ni miongoni mwa maneno yanayokatisha tamaa mabondia wa kike kuingia katika mchezo huo

Mdau Raheli Elias na Harufu ya kikwapa
Harufu ya kikwapa imekua tatizo kubwa kwa jamii yetu na
watu wengi wameizoea hiyo harufu kiasi kwamba hawajitambui kua wanatoa harufu. Watu
wengi wa nchi za nje wakija Tanzania wanalalamika kua harufu ya kikwapa
inawasumbua.

Harufu ya kikwapa inatokana na
sababu nyingi kama usafi wa mwili, chakula kama (Red meat). Mtu anapotoa jasho,
bacteria wanatumia nafasi hiyo kwenda kwenye jasho kujipatia chakula. Kadri
bacteria wanavyokua wengi, harufu nayo inazidi. Kuoga kunasababisha bacteria
kuondoka hasa kama unatumia sabuni inayoua hao bacteria (antiseptic soap).
Bacteria wanaokaa kwenye kikwapa wanazidi pia kama unatumia kitaulo cha kuogea
na kutokukifua vizuri na kuacha kisikauke. Hivyo unashauriwa kukianika nje
kikauke baada ya kuoga, pamoja na taulo ya kujifutia ili viondokane na bacteria
au kama inawezekana kufua kila siku.

Kwa sababu mtu hawezi kushinda
anaoga siku nzima ni bora kutumia njia za kukinga harufu ya kikwapa. Njia hizo
ni kama zifuatazo:

1.
Kutumia
deodorants au antiperspirants.
Deodorants zinasaidia kuondoa bacteria ambao wako kwenye kikwapa. Mara nyingi
hua zina harufu nzuri na kuna ambazo hazina. Kazi yake ni kufanya bacteria
wasikae kwenye kikwapa. Antiperspirants zinazuia jasho lisitoke kwa wingi.
Unapoenda kununua deodorant angalia yenye ingredient inayoitwa Aluminium chlorohydrate.

2.
Kutumia baking powder. Hii ni njia rahisi zaidi ambayo
inatumia gharama ndogo zaidi. Kuna
packet ya baking powder ambayo inauzwa bei chini ya shilling mia na itadumu kwa
muda hata wa miezi mitatu. Weka kidogo kwenye kiganja, changanya na maji halafu paka kwenye kikwapa baada ya kuoga.
Hii itazuia harufu ya kikwapa siku nzima.

3.
Vaa
nguo za kitambaa cha cotton au wool. Nina maana kwamba nguo ambazo ni synthetic
kappa polyester au nylon zinafanya mtu atoe jasho zaidi.

4.
Nyoa
nywele za kikwapa. Nywele zikiwa nyingi zinakua kama mtego wa bacteria na
kusababisha harufu.

5.
Kunywa
maji mengi. Maji yanasaidia kutoa sumu kwenye mwili na kusababisha harufu
kupungua.

6.
Oga
angalau mara mbili kwa siku na kusugua vizuri sehemu ya kikwapa.

7.
Vaa
nguo safi kila siku.
Vaa
nguo safi kila siku.
8.
Hakikisha
huna harufu ya kikwapa kabla ya kutumia perfume kali. Mchanganyiko wa harufu ya
kikwapa na perfume inatoa harufu mbaya zaidi.

CHADEMA WADAIWA KUFANYA USANII
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM),kimesema kimeshangazwa na kusikitishwa na usanii unaofanywa
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwahadaa Watanzania kwa
usanii wa kufanya harambee kuhalalisha uwepo wa mabilioni waliopewa na
wafadhili wao kutoka nje ya nchi.

Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama cha Mapinduzi, Nape Nnauye, alisema huo umekuwa ni utamaduni wa chama
hicho kuwahadaa watu kwa kuitisha za kisanii baada ya kupewa mabilioni na wafadhili.

Alisema itakumbukwa mara kadhaa Chadema
wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii na kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya
Watanzania kwa kuwaomba wakichangia chama hicho huku wakati huo tayrai
wameishapata mabilioni toka kwa wafadhili wao.

Alisema
kwa mfano mzuri wa usanii huo ni hivi karibuni kwenye haoteli ya Serena ambapo
ilifanyika harambee na kurushwa na moja kwa moja naKituo kimoja cha
Televisheni.

Nnauye
alisemaa umekuwa utamaduni wa chama hicho kuwahadaa watu kwa kuiitisha harambee
za kisanii baada ya kupewa mabilioni na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe
kuwa pesa wanazotumia zimetokana na michango ya Watanzania wakati siyo kweli.

“Tunao
ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chademajuzi na wafadhili
hao kwa lengo la kuendeleza operesheni mbalimbali nchini.

“Cha
kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania ukweli wa haya
mabilioni wanaanza kuwahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato haya mtaji wa
baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”alisema Nnauye.

“Hebu
tujiulize, kwa nini mabilioni haya yanatolewa kwa Chadema sasa ambapo nchi yetu
imeendelea kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwemo gesi
na mafuta?”

nchi nyingi hasa zinazoendelea zenye utajiri wa wa rasilimali mbalimbali zimekumbwa
na migogoro ya ndani isiyokuwa na kichwa wala miguu na kushuhudia rasilimali
zao zikivunwa na kuporwa bila huruma wala simile ambapo wakati huo wananchi
wakiachwa masikini wa kutupwa na wahanga wa vita hizo zinazonufaisha wakubwa.

Aidha,
wamekitaka Chadema kuweka wazi mashart yanayoambatana na mabilioni hayo, waseme
hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na waache mara moja kuwahadaa
watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni chama cha wanyonge kinachotegemea
kujiendesha kwa michango ya watanzania.

alibainisha kuwa iwapo Chadema hawatawaeleza ukweli wananchi basi chama chake
kitawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni hayo,
walikozitoa na mikataba walioingia.

lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa nchi haiwekwi reheni kwa uroho wa madaraka wa
baadhi ya wanasiasa.

SERIKALI KUBEBA JUKUMU LA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA TAZARA
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk Harryson Mwakyembe amesema serikali itabeba jukumu la kulipa
mishahara ya wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA, baada ya
wafanyakazi hao kucheleweshewa mshahara yao kwa kipindi cha miezi mitatu.
Kauli
hiyo imekuja baada ya wafanyakazi wa shirika hilo kufikisha kilio chao kwa
Waziri huyo kuwa wamekuwa wakiishi maisha ya kubangaiza kutoakana
ucheleweshwaji wa mishahara yao.

na wafanyakazi hao, kwenye ofisi za Shirika hilo (TAZARA), jijini Dar es salaam
jana, Dk Mwakyembe alisema akiwa waziri wa wizara hiyo anawaahidi hatakubali
kuona wanaishi bila kulipwa mishahara huku wakifanya kazikwa juhudi.

Dk
Mwakyembe alibainisha kuwa serikali imepokea kilio chao hivyo italipa sh
bilioni1.3 kama mshahara wa miezi miwili kati ya miezi hiyo mitatu wanayodai
kuanzia leo (jana).

Aliitaja
miezihiyo itakayolipwa kuwa ni pamoja na Juni na Julai ambapo amewataka
viongozi wa Shirika hilo kutoa maelezo kuwa ni kwanini hadi sasa hawajalipa
mishahara wafanyakazi hao.

Akizungumzia
madai ya wafanyakazi hao ya kutaka kung’olewa madarakani kwa Mkurugenzi Mkuu,Mbegusita Akashambatwa
na Naibu wake, Damus Ndumbalo, alisema shirika hili ni la kimataifa
linalohusisha nchi mbili hivyo maamuzi yake ni lazima ya husishe viongozi wa
pande zote mbili.

alitoa onyo kuhusu vitendo vya hujuma ikiwa ni pamoja na wizi kuwa wale wote
wanaojihusisha watambuwe kuwa dawa yao iko jikoni inachemka.

Katika
hatua nyingine amesema amesikitishwa sana kuona kuwa wafanyakazi wa Mradi wa
Ukarabati wa Train Mijini, hadi leo hawjalipwa mishahara ya miezi miwili,fedha
hizo lilikwishatengwa.

“Nilisikitika
sana kumkuta yule dada Mwanamisi akiwa amevaa overrol lake huku akiunganisha
vyuma tena amefunga mfungo wa Ramadhani ambapo aliniambia tunafanyakazi lakini
hatujalipwa mishahara inishangaza sana nataka walipwe haraka”alisema Dk
Mwakyembe.

Awali
Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi shirika hilo, Ernest Kiwele, alisema
wamechoshwa na tabia za viongozi hao kuwa wamekuwa chanzo cha matatizo yote
yanayowakabili wafanyakazi hao.

Mkurugenzi Mkuu na Naibu wake wamekuwa wakiendesha Shirika hilo kwa kujali
zaidi maslahi yao na jamaa zao hata wale waliosimamishwa kazi kwa kuwalipa
mishahara.

RECENT COMMENTS