BENDI YA MSONDO NGOMA YATANGAZA RATIBA YA WIKI

BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika wiki baada ya mpambano wao mkali na mahasimu wao Sikinde uliofanyika Jijini Dar es salaam pamoja na Zanzibar.

Baada ya kutoa burudani ya Iddi sasa wamerudi kwa ajiri ya kutoa burudani  ambapo wamesema kuwa wataanza kutoa burudani siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi watakuwa  Kilimani Pub Staki Shari, na jumapili watamaliza wikiendi katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni

 Akiongea  na Fullshangweblog Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini kinachoendelea baada ya kusherekea sikukuu .

 “Msondo ipo kamili katika kutoa burudani na ndiyo maana imeamua kutoa ratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye maonesho yetu kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema Super D.

Alitaja vibao vinavyotamba kwa sasa vya bendi hiyo kuwa na Suluhu wa Sabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga mbali na nyimbo hizo bendi hiyo itapiga nyimbo zake zilizotamba zamani zikiwemo Asha Mwanasefu,Cheusi Mangara,mwana Mkiwa na nyingine nyingi zilizotamba kipindi hicho
MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!