MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AKUTANA NA MKURUGENZI WA BODI YA UTALII (TTB)

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema akimsikiliza mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB), Dkt Aloyce K. Nzuki wakati akimuonesha mpango wa kuendeleza Bustani ya Posta kwa ajili utalii wa utamaduni, katika mazungumzo yao wakati mkuu wa wilaya huyo alipotembelea katika ofisi za bodi hiyo zilizopo jengo la (IPS) jijini Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kuangalia uwezekano wa  kukuza utalii  katika Wilaya ya Temeke na maeneo mengine ya jiji la Dar bes salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema wa tatu kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB) Dkt Aloyce K. Nzuki, mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kwenye ofisi za taasisi hiyo. Pichani ni  baadhi ya watendaji  wa bodi hiyo, kulia ni Geofrey Meena,  Meneja Masoko wa TTB; na wengine kutoka kushoto ni Serenga Kaduma, Mwanasheria wa TTB; na Philip Chitaunga, Meneja wa Huduma za Utalii.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!