MKUU WA WILAYA YA MUHEZA AHAMASISHA ZOEZI LA SENSA NYUMBA KWA NYUMBA

MKUU wa wilaya ya Muheza Tanga, Subira Mgalu ametoa kali ya mwaka baada ya kuhamasisha Sensa ya watu na Makazi kwa aina yake baada ya kupita nyumba kwa nyumba usiku.

 Pia mkuu huyo wa wilaya amekuwa akipita katika masoko mbalimbali na hatimaye kuwahubilia wafanyabiashara kuwa wajitokeze katika kuhesabia Sensa hapo Agusti 26 jumapili ijayo.
 Ikiwa hiyo haitoshi mkuu huyo amekuwa akikata mitaa mbalimbali kwa miguu na kuwasimamisha wanaume,wanawake na watoto akiwahamasisha kujitokeza katika Sensa ya watu na makazi.
 Akiwa katika soko kuu wilayani hapa juzi mkuu huyo wa wilaya alionekana akipiga kampeni yake sokoni humo kwa kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kukamilisha kazi hiyo ya kuhesabiwa siku hiyo ya  jumapili ijayo.
 Mgalu aliwaomba wafanyabiashara hao kuwa itakapofika siku ya kuhesabiwa wasitoke nyumbani mpaka wahesabiwe.
 Alisema kuwa watafika makarani wa SensA mpaka katika nyumba husika na watatoa maelekezo kwa wananchi hao kuhusu Sensa hiyo.
 Mgalu alisema kuwa Sensa ni muhimu sana kwa kuwa serikali itajua idadi ya watu wake na hivyo kuiwezesha kupanga mipango yake ya maendeleo kwa wananchi wake.

 

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!