Gladness Mushi wa Fullshangweblog-Arusha
MAANDALIZI ya zoezi la sensa ya kuhesabu watu na makazi kwa mkoa wa
arusha yamekamilika vya kut osha ambapo jumla ya makarani elfu 5037
wamechaguliwa kuendeleza shughuli hiyo sanjari na kukamilika kwa vifaa
mbali mbali vitakavyotumika katika zoezi hilo.
Hayo yamebinishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya zoezi hilo la Sensa kuhusiana na
Mulongo alifafanua kuwa matayarisho ya sensa yameshaiva na kuwa tayari ambapo watu muhimu wakiwemo makarani tayari wameshapatiwa mafunzo halisi ya juu ya zoezi hilo.
Aliongeza kuwa jumla ya maeneo 3290 tayari yameshatengwa kwa ajili ya
kuendesha zoezi hilo ambapo alisema kuwa makarani hao wameshaanza
kupita ili kuonana na viongozi mbali mbali ili wabaini ukomo wa maeneo
yao watakayokuwa wanayafanyia kazi.
Mulongo alisema kuwa pia kukamilika kwa maandalizi ya zoezi hilo
kumetokana na mafunzo waliyoyatoa kwa madiwani ,viongozi wa dini
pamoja na viongozi wa vyama vya siasa ambapo makundi haya yamesaidia
kwa kiwango kikubwa katika kuhamasisha watu ili washiriki katika zoezi
hilo.
Aidha aliwataka wale watu wote wenye nia mbaya ya kuwatisha makarani
hao wawapo kwenye zoezi hilo kutambua kuwa ulinzi utakuwepo kwa kila
eneo husika na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria
kwa kuwa zoezi hilo sio la mtu binafsi bali ni la kitaifa.
Pia aliwataka wanannchi wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanashirki ipasavyo katika zoezi hilo la Sensa kwani sensa ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa la tanzania na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.









