NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWEBLOG-ARUSHA
TANZANIA itakuwa ni mwenyeji wa mkutano wa kumi na nne wa mazingira
kwa nchi za Afrika utakaonza Rasmi September 10 mpaka 14 mwaka huu
ndani ya mkoa wa Arusha
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo alisema kuwa
mkutano huo utaweza kuwakutanisha maelfu ya wananchi sanjari na
mawaziri wan chi hizo
Bw Magesa alisema kuwa kwa mkutano huo utaweza kuwaweka sehemu moja
wananchi pamnoja na mawaziri ambao wanahusika na mazingira kwa nchi
hizo huku lengo halisi likiwa ni kujadili mambo mbalimbali yahusiyo
mazingira
Alifafanua kuwa mbali na hayo mwenyeji wa mkutano huo atakuwa ni
Raisi Jakaya kikwete ambapo mkutano huo pia utakuwa na faida kubwa
sana kwenye jamii hasa za mkoa wa Arusha
Aliongeza kuwa ni fursa ya wananchi wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa
wanajipanga ilivyo katika kuwapokeas wageni hao ambapo kabla ya kuanza
ka mkutano huo pia utatanguliwa na mkutano mwingine wa wadau wengine
wa mazingira ambao nao wataweza kujadili changamoto mbalimbali ambazo
zinaikabili sekta hiyo ya Mazingira hasa kwa nchi za Bara la Afrika.








