WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AENDELEA NA MKUTANO WA TISA WA SULLIVAN, MALABO EQUATORIAL GUINEA

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Ghana Bw. John Kufuor mjini Malabo, Equatorial Guinea (Picha na Pascal Shelutete)

 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Ghana, John Kufuor ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha Utawala Bora katika nchi za kiafrika. Aidha, Rais Mstaafu Kufuor alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Jakaya Kikwete aliyefika nchini Ghana kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo John Atta Mills na kusema kuwa ni ishara ya uhusiano wa kidugu uliopo baina ya Tanzania na Ghana tangu enzi za waasisi wa mataifa haya Kwame Nkrumah na Mwalimu Julius Nyerere. (Habari Picha na Pascal Shelutete) 

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!