Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
WAMILIKI wa Vyuo Binafsi kwa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wafanyakazi wenye sifa kwani endapo kama watatoa ajira kwa watu ambao hawana sifa ni wazi kuwa watakuwa ni chanzo cha Umaskini hasa kwenye sekta ya ajira binafsi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Diwani wa kata ya Ngarenaro Bw Isaya Doita wakati akiongea katika maafali ya pili ya chuo cha Hoteli cha Fountain Justice Training College(FJTC) kilichopo Sakina mjini hapa
Bw Doita alisema kuwa vyuo Binafsi vina nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia maendeleo ya jamii hasa pale ambapo kama watatoa ajira kwa watu wenye sifa lakini pia vyuo hivyo vina wezakuwa Chanzo cha kukosa ajira hasa pale ambapo wataajiri watu ambao hawana sifa maalumu ya kufundisha katika vyuo hivyo
Alisema kuwa Kamwe vyuo vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya mitaa havipaswi kuona kuwa havina mchango kwa jamii badala yake vyuo hivyo vinatakiwa kujijenga na kujiimarisha zaidi ili view ni chachu ya mafanikio hasa katika suala zima la Ajira hapa Nchini
Alifafanua kuwa kama Vyuo vyote vitalenga kuwa na mitaala ambayo inakubalika ndani ya jamii basi mbali na kutoa ajira kwa wanafunzi ambao wanaitimu katika vyuo hivyo basi vitachangia sana wanafunzi kuweza kujiajiri wao wenyewe na kuachana na tabia ya kusubiri kuajiriwa wakati uwezo wa kujiajiri wao kama waitimu upo
“kwa sasa vipo baadhi ya vyuo ambavyo vinaajiri hata walimu ambao hawana uwezo wakidhani kuwa hawaonekani na jamii lakini wajue kuwa wao wanachangia sana umaskini kwenye jamii yetu kwani Lengo la hivi Vyuo ni kuhakikisha kuwa vinaboresha maisha ya Watanzania kwa maana hiyo ni vizuri kama kila Mkurugenzi wa chuo akahakikisha kuwa anatoa msaada kwa jamii na wala sio kuwa chanzo cha Umaskini”aliongeza Bw Doita
Awali Mkuu wa chuo hicho Bw Justice Wilson alisema kuwa Chuo hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa kinatoa elimu bora zaidi hasa ya ngazi ya Hotelia kwani kupitia fani hiyo wanafunzi wanaweza kujiajiri huku wakiwa ni chanzo pekee cha kuimarisha zaidi sekta ya Utalii huku pia wakiweza kuepusha Nchi na majanga mbalimbali ya uhaba wa ajira.
Aliongeza kuwa mbali na hayo bado wanafunzi ambao wanaitimu katika mafunzo hayo bado wanakabiliwa na changamoto mbalimnbali hasa za udhalilishaji hali ambayo inafanya wengi wao kuishia njiani bila kufikia malengo yao mbalimnbali
“Pamoja na kuwa sisi kama sisi tunawasaidia kuwapa elimu hawa Vijana lakini kule wanapoenda wanajikuta baadhi ya wamiliki wa hoteli ambao hawana maadili wanawalazimisha kufanya kile ambacho kipo nje ya masomo sasa hali hii ni changamoto na tunataka hili liishe wapate haki zao za msingi kwa kuwajibika vema kama ilivyo lengo la Vyuo kama hivi”aliongeza Bw Justice








