MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASHIRIKI ZOEZI LA SENSA JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia) ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi, lililoanza  leo nchini kote, ambalo litadumu kwa siku saba. Picha na OMR
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti 26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Dkt. Bilal, ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.
 Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37, yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
 Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo, ambalo litadumu kwa siku saba.
MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!