SHIRIKA la Kutetea Uhai wa Binadamu nchini (PRO-LIFE), limewataka Watanzania kuwa makini katika matumizi ya dawa za vizibiti mimba,lengo lake likiwa nikupunguza idadi ya watu ili mataifa makubwa yaendelee kupora rasilimali za Waafrika.Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti wa Elimu kutoka nchini Marekan, Brian Clowes, alisema Tanzania haina haja ya wananchi wake kujiingiza katika kampeni hiyo wa vidhibiti mimba, Tanzania bado inaidadi ndogo ya watu ukilinganisha na mataifa mengine duniani.
Alisema kampeni hiyo, lengo lake ni kuzuia ongezeko la watu, ili mataifa hayo makubwa yaweze kuendelea kuyaibia rasilimaali zao Watanzania na nchi nyingine za afrika ambapo ongezeko la watu katika nchi hizo ni kikwazo kwao.
“Fedha za Kampeni za uzazi wa mpango zimekuwa zikielekezwa kwenye nchi ambazo kwa kiasi kikubwa zinaongezeko la watu haswa maeneo yenye watu weusi”alisema Clowes.
Clowes alisema hivi sasa nchi nyingi za ulaya zimekumbwa na hofu ya kuwa na wazee wengi ukilinganisha na nchi za Afrika ambapo zinaonekana kuwa na vijana wengi.
Alisema mwaka 1950, Ulaya ilikuwa na asilimia 22 ya watu ambapo Bara la Afrika lilikuwa na asilimia 9 hali inayoonesha kuwa Bara hilo lilikuwa tupu.
Clowes alisema mwaka 1960, Bara la Ulaya lilitangaza kampeni ya kudhibiti mimba ambapo hadi mwaka 1997, idadi ya watu katika Bara hilo imezidi kupungua na inakadiriwa ifikapo mwaka 2050, litakuwa na asilimia nane ya watu huku Bara la Afrika idadi yake ya watu ikiongezeka na kuwa asilimia 21.
Akizungumzia vidhibiti mimba, kingaa ya gonjwa la Ukimwi alisema siyo kweli kama kondom inauwezo wakuzuia ukimwi na mimba bali kampeni hizo zina lengo la kuvinufaisha viwanda kibiashara.
“Wakati zamani mataifa hayo ya Ulaya yakitumia vifaru, bastola, bunduki na ndege kuzitwala nchi hizo za kiafrika na nyingine dunia hivi sasa zimekuja na ukolino mamboleo kwa uiaminisha jamii kuwa maisha mazuri yanatokana na upangaji uzazi ambapo matumizi dawa hizo yamekuwa na athari mbaya kwa wakina mama pamoja na kuua watoto wanaotarajiwa kuzaliwa”alisema Clowes.
Naye Mkurugenzi wa shirika hilo, Emmil Hagamu, alisema jamii inapaswa kutumia njia za mpango wa uzazi za asili ambazo hazina madhara.
Alisema haamini kama matumizi ya kondom na madawa mengine kuwa ni njia salama za kudhibiti mimba na kupunguza maambukizi ya maradhi ya ukimwi.
Hagamu aliitaka jamii kutambua kuwa nchi nyingi zilizojiingiza kwenye matumizi ya kondom ndizo zimekuwa zikiongoza kwa maambukizi ya ukimwi kutokana na kondom nyingi kuwa hazifanyi kazi tangu zikiwa kiwandani.
Alitoa wito kwa kuitaka jamii kubadili mitazamo katika kujiepusha na ngono zembe kama wanavyoishi watu wenye mitazamo ya kidini kutoka Afrika ya kasikazini ambapo wanaamini ndoa ndiyo dawa ya kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi.








