
KITUO CHA UTAMADUNI NA MAENDELEO YA VIJANA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA STUDIO YA MORO TOWN RECORD WAMEANDAA TAMASHA LA KUKUZA VIPAJI MKOANI MOROGORO.
TAMASHA HILO LINALOSHIRIKISHA VIJANA 250 KUTOKA MKOA WA MOROGORO,PWANI NA MAENEO YA HKARIBU YALIANZA JANA MJINI MOROGORO,
LENGO LA TAMASHA HILI NI KUKUZA VIPAJI.AMBAPO WASHINDI WATAPATA BAHATI YA KURECORD ALBUM MOJA MOJA NA WASHINDI KWA UPANDE WA MAIGIZO WATAPATA BAHATI YA KUREKODI FILAMU,
SHINDANO HILO LITAKUWA LINARUSHWA MOJA KWA MOJA NA TELEVISION YA ABOOD YA MJINI MOROGORO ILI KUWAPA WATAZAMAJI FURSA YA KUWAPIGIA KURA WASHIRIKI
Washiriki wa maigizo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchujo katika tamasha hilo la kukuza vipaji mkoani morogoro
Washiriki wa kuimba wakiwa katika picha ya pamoja
Washiriki wa shindano hilo Paulo Lucas na Denis wakiwa katika pozi kabla ya shindano hilo kuanza jana mkoani morogoro







