WAKULIMA nchini huenda wakaingia kwenye umasikini wakutisha kutokana na uchakachuaji wa pembejeo unaofanywa na baadhi ya wa Waingizaji na Wasambazaji wa pembejeo na dawa za mifugo hizo.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki, na wadau wa usambazaji mbolea, viuatilifu na madawa ya mifugo kwa wakulima wadogo wadogo, waliyoshiriki washa ya siku moja kujadili Ripoti ya utafiti iliyofanywa na Baraza la Kilimo (ACT), hivi karibuni.
Walisema tatizo hilo la uchakachuaji wa madawa na utengezaji wa mbolea bandia limekuwa likienea kwa kasi kubwa, karibu nchi nzima hali inayoashiria kuharibu udongo na kuua mazao yote yanayo mwagiliwa mbolea na madawa hayo.
Mmoja wa washiriki wa washa hiyo, Suleiman Khamisi, salibainisha kuwa tatizo hilo ni kubwa na kama serikali haita kuwa makini katika kulidhibiti kuna hatari nchi hii ikaja kukumbwa na janga la njaa.
“Viongozi wetu wanapaswa walione hili na kwa pamoja tu tuelekeze nguvu zetu kama ilivotokea kwenye vita ya uchakachuaji wa mafuta ambapo ili saidia kupunguza tatizo hilo japo kwa kiasi”alisema Khamisi.
Alisema kutokana na wakuliama kutokuwa na utaalamu wa kutambua mbolea au dawa ipi ni badia wanalazimika kuzinunua bila kujua madhara yatakayojitokeza baadaye.
Khamisi alisema pembejeo hizo zimekuwa zikiwatia hasara wakulima wakati wa mavuno, hivyo kuwaingiza kwenye migogoro na taasisi za fedha kutokana na kukosa fedha za kulipa mikopo waliyokopa kwa ajili ya kilimo.
Pia vitendo hivyo vinaathili soko la nje kwa kuwakimbiza wafanyabiashara wanje kuacha kuja kununua pembejeo hizo badala yake kuhamia nchi nyingine.
Awali Mtaalamu Mwelekezi, Edmund Ringo, alisema tatizo hilo la uchakachuaji pembejeo na viuatilifu limejitokeza katika maeneo mbalimbali walioyafanyia utafiti, inaonyesha tatizo hilo liko karibu nchi nzima.
Alisema kuwa vitendo hivyo, vimekuwa vikifanywa na baadhi ya makundi ya watu wenye tama ambapo kukomesha hali hiyo, kunaulazima kwa Baraza hilo kutunga sera ambayo italinda maslahi.





