Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya 10 ya jumuia ya wahandisi kuanzia tarehe 6-7 mwezi wa tisa mwaka huu. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kulia ni Msajili wa Bodi Mhandisi Steven Mlote.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo)
Msajili wa Bodi ya wahandisi nchini Mhandisi Steven Mlote akijibu maswali ya waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Bodi hiyo iliweza kuwafutia usajili wahandisi 164 ambao walikiuka maadili ya kazi na kusimamisha miradi 12 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za uhandisi na taratibu za kiujenzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.
Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa wahandisi nchini Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu sherehe za maadhimisho ya 10 ya jumuia ya wahandisi yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City kuanzia tarehe 6-7 mwezi wa tisa mwaka huu. Kulia ni Msajili wa Bodi Mhandisi Steven Mlote na Kushoto ni Msajili Msaidizi Mhandisi Benedict Mukama.




