Wanaoafundisha wananchi jinsi ya kuchangia katiba mpya wanaharibu:Jaji Warioba

Na Gladness Mushi,Arusha

 TAASISI na Mashirika mbalimbali ambayo yanawafundisha wananchi jinsi ya kuchangia moni yao kwenye suala zima la katiba mpya wanapotosha maana halisi ya Uhuru wa Mtanzania na wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwani hapo baadaye Taasii hizo kwa umoja wao watapewa nafasi ya kuchangia

MWENYEKITI wa Tume ya Katiba mpya hapa nchini Jaji Sinde Warioba ameyasema hayo mjini Arusha wakati akifungua mkutano kwa wanachama wa chama cha wanasheria cha Tanganyika (TLS)

 Jaji Warioba ameeleza kuwa ni vema kama Makundi hayo ya kijamii yakajua kuwa yanawakandamiza wananchi kwa kushindwa kuwapa haki zao za msingi na kwa kufanya hivyo watasababisha malengo halisi ya Tumehiyo  na hivyo bado jamii itabakiwa na changamoto hizo hizo

 Jaji huyo aliwataka wanasheria hao kuhakikisha kuwa wanachangia Katiba mpya kwa kuhamasisha wananchi wote hata wale ambao hawana elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa Katiba mpya kwa maisha ya hapo baadaye hasa pale ambapo Katiba ya sasa itavunjwa.

 Pia alisema kuwa nao Wanasheria wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri hasa katika kutangazia Umma umuhimu wa kushirikii na kuchangia Katiba mpya kwani Katiba na Sheria havipangani bali vinaendana kwa pamoja

 Naye Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla alisema kuwa ili kukabiliana na masuala mbalimbali ambayo yanajitokeza katika Katiba, wanachama wa chama hicho Watajadili kwa pamoja ambapo mara baada ya majadiliano watatoka na maazimio mbalimbali ambayo yatalenga kujenga na kuimarisha  Mchakato mzima wa Katiba mpya

 Bw Stolla aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kulinda Umma wa Watanzania kutokana na hali hiyo wadau wa Sheria  wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia Serikali hasa katika zoezi la Ukusanyaji wa Maoni yahususyo Katiba mpya.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!