MZEE YUSSUF AFUNGUA KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA KAZI ZAKE

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kufungua kampuni yake ya usambazaji ijulikanayo kama MY Collection kwa ajili ya kusambaza kazi zake

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Mussa Msuba amesema wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya Jahazi inayongozwa na Mzee Yussuf duka hilo lililopo makutano ya barabara ya likoma na Muhonda

Duka hilo litauza  DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya kuwaweka karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo zao kwa kuwaburudisha wakiwa majumbani

Msuba amesema kuwa Mzee Yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake ya mduara itakayokuwa hivi karibuni ambayo ni yake binafsi mbali na hilo bendi hiyo itatoa video yake ya Live za albamu zake zote za Two in One,Kazi ya Mungu, Nakula ka Naksh Naksh,tupendane,Daktari wa Mapenzi

Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao

Nae Mzee Yussuf aliongeza kwa kusema ameanzisha Kampuni yake binafsi baada ya kuona kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo kwa wizi wa kazi za Sanaa

Kampuni yake imekuwa ikisambaza kazi zake kwa ajili ya kuogopa kuibiwa kutokana na wimbi wa kazi za wasanii nchini

Duka lililopo mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee  mbali na duka hilo mzee Yusufu anamiliki Duka lingine la Nguo lililopo Magomeni Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake mbali na bendi yake

Bendi ya Jahazi mpaka sasa imekwisha toa albam nane ambazo zipo madukani zinauzwa kwa maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa sasa bendi hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa ambayo haijapewa jina inatarajiwa kuzinduliwa mwezi Oktoba mwaka huu Mzee Yusuf amewataka mashabiki  wao kuja kuangalia na kusikiliza nyimbo mpya popote pale wanapofanya maonesho yaokatika kumbi mbalimbali za jijini Dar es salaam

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!