TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LAVUNJA REKODI YA MOSHI NA TANGA WAKAZI WA MUSOMA WAPAGAWA, LEO NI CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

Profesa Jay Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva akifanya vitu vyake jukwaani kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma juzi Ijumaa.

Baada ya kufanya vizuri sana mikoa ya Kilimanjaro katika viwanja vya chuo cha Ushirika Moshi na uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga, tamasha la Serengeti fiesta sasa limehamia kanda ya ziwa kwa kishindo ambapo juzi ijumaa Serengeti fiesta iliangusha burudani ya aina yake mjini musoma na kuwafanya mashabiki wa tamasha hilo wafurike katika uwanja wa Karume mkoani Mara  kufurahia burudani kali kutoka kwa wasanii wa bongo flava.

Pamoaja na ukweli kwamba tamasha la Serengeti fiesta lilikuwa likitoka Musoma linaelekea Shinyanga na baadaye kubisha hodi ndani ya jiji la Mwanza, bado shamrashamra zote siku ya juzi ijumaa zilielekea huko Musoma zikianzia Mwanza, Shinyanga, Tarime, na vitongoji vya jirani.

Tamasha hilo kubwa kuliko matamasha yote hapa nchini na eneo la Africa mashariki lilipambwa na burudania kali kutoka kwa wasanii kama vile Chege, mheshimiwa Temba,bibi Cheka,Recho,Bob Junior, Fid Q, At, Omi Dimpoz, Mwasiti,Ney wa Mitego, Barnaba, Prof Jay na wengine wengi.

Vumbi kubwa liliinuka na kutanda juu ya anga za uwanja wa Karume mjini Musoma baada ya washindi wa Serengeti fiesta supa nyota 2012 kupanda jukwaani kwa kishindo cha aina yake na kwa kupiga wimbo uliwainua mashabiki wote na kuanza kusakata muziki kila mtu na staili yake huku wasanii wa filamu za kibongo Vicent Kigosi maarufu kama Ray, Steve Nyerere,JB,na Anti Ezekiel wakiuongezea ladha tamasha hilo kwa kucheza kiduku na kuwapandisha mzuka mashabiki wa Serengeti fiesta waliojikuta wakikanyagana kutokana na kila mmoja kutaka kuwaona wasanii hao kwa ukaribu na hata ikiwezekana kucheza nao.

Akiongea na wanahabari waliohudhuria tamasha hilo, meneja wa mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya ziwa Bw. Patrick Kisaka amesema “Tamasha la Serengeti fiesta mwaka huu Musoma limepokelewa kwa mwitikio wa kipekee tofauti na jinsi ilivyozoeleka miaka iliyopita na kwamba Serengeti fiesta 2012 mwaka huu ina zawadi maalum kwa watanzania wote hasa mashabiki wa Serengeti fiesta watakashiriki bahati nasibu ambayo mshiriki atapata kujishindia gari aina Toyota Vitz na pikipiki na jinsi ya kushiriki ni kuandika neno Serengeti fiesta 2012, unaacha nafasi sehemu inakofanyikia mfano musoma, kisha tuma kwenda namba 15555” alisema Kisaka.

Kwa upande wake meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, akiongea kwa njia ya simu katika mahojianoa na waandishi wa habari, Bw. Allan Chonjo amesema wakazi wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi kushiriki katika tamasha la Serengeti fiesta kwani mbali na kuleta burudani na kujenga mahusiano mazuri kwa vijana, pia linalenga kuinua vipaji vipya katika tasnia ya muziki hapa nchini pamoja kuboresha maisha kwa watanzania kupitia zawadi zinazoshindaniwa kupitia Serengeti fiesta 2012.

Ni mwaka wa nne sasa tangu kampuni ya bia ya Serengeti ianze kudhamini tamasha la Fiesta ambapo mpaka sasa wasanii mbalimbali wa kizazi kipya wameweza kutoka kimaisha na wengine kupiga hatua kimaisha kupitia filamu za kibongo. Katika matamasha ya Serengeti fiesta watanzania wengi wamekuwa wakijipatia riziki mbalimbali kutokana na fanyika kwa biashara mbalimbali kama vile kuuza chakula, vinywaji baridi, nguo, nyumba za kulala wageni pamoja biashara niyingine nyingi kufanyika kwa wingi na kwa faida siku na mahali ambapo tamasha limepita.

Baada ya  Musoma tamasha Serengeti fiesta 2012 jana jumamosi  limefanyika mjini Shinyanga  na kumalizia kanda ya ziwa kwa kuangusha buruda kubwa jiji Mwanza siku ya leo jumapili tar.2/08/2012 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Kutoka kanda ya ziwa, Serengeti fiesta itaelekea mikoa ya Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya, Zanzibar na baadaye fainali itafanyika katika jiji la Dar Es Salaam, hivyo wakazi wa maeneo hayo wakae mkao wa kula kwani Serengeti fiesta 2012 inakuja.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!