Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wagonjwa wa saratani waliolazwa katika wodi hospitalini hapo. Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Twalib Ngoma alisema hivi sasa watanzania 100 wanafariki kwa ugonjwa wa saratani na asilimia 35 ya ugonjwa huo unaweza kuzuilika.
Mh. Dkt. Mwinyi akipata maelezo toka kwa mtaalam(hayupo pichani) wa mashine inayosaidia kuchanganya dawa za mionzi na kuchunguza wagonjwa mbalimbali ( Nuclear Medicine)iliyopo katika jengo jipya la hospitali ya Ocean Road.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika chumba cha mionzi. Idadi ya wagonjwa wa saratani imeongezeka toka wagonjwa 2,000 mwaka 2002 hadi kufikia wagonjwa 5,000 hivi sasa.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road wakimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwenye ukumbi wa Mkutano hospitalini hapo.Picha zote na Catherine Sungura-MOHSW)




