Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha kulia.
(NA GLADNESS MUSHI,ARUSHA)
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, Wilaya ya Arumeru, Ester Maleko, ameukwaa Ueenyekiti wa Jumuia ya Wanawake UWT, Wilaya ya Arusha DC, baada ya kuwabwaga wagombea wenzake watatu ambao wawili walijitoa katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa kikali.
Katika Uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa shule ya msingi Green Acre,na kusimamiwa na Katibu wa CCm, wilaya ya Meru, Langael Akyoo, Mwenyekiti huyo alipata kura 207 na kuwashinda Diwani wa viti maalumu, Penina Mollel, aliyepata kura 72 huku wagombea wengine Agness John Molle,alipata kura 3 na Alfrida John Laizer, kura 2 waliojitoa .
Ester Maleko, anaandika histori wilayani humo kuwa mwenyekiti wa kwanza kijana ,aliyotoka UVCCM na kuukwaa uenyekiti wa UWT, wa Wilaya hiyo, kuliko wote na kwa kupata kura nyingi zaidi Nafasi ya mkutano mkuu wa CCm taifa ilichukuliwa na Yasimin Bacho, aliyepata kura 243, Agness Molle, aliyepata kura 172 na Magdalena kokan, mwenyekiti wa UWT, aliyemaliza muda wake aliyepata kura 143
Nafasi ya mkutano mkuu wa CCM,mkoa ilichukuliwa na Egmeller Laban, aliyepata kura 34 na kumbwaga Margreth Mongi, aliyepata kura 14, Nafasi ya Halmashauri kuu Wilaya ilichukuliwa na Neema long’ida aliyepata kura 194 na kumbwaga Anna Mushgi aliyepata kura 82.Nafasi ya
Nafasi ya Mkutano mkuu wa CCM, wilaya imeshukuliwa na Beather Lukumay,alipata kura 250 alimshinda Margareth Mongi, aliyepata kura 28 .
Mkutano mkuu wa UWT, Mkoa nafasi zilikuwa tatu zilichukuliwa na Apaililia Daniel ,Malinda Mathew, na ndeneng’o Mollel, Nafasi ya Baraza kuu UWT, wilaya ni Suzan Kichao, (263) Agness mbise(244), Elizabeth Daud,(244) Nay Molle(241) Magdalena kokan (236)Ndanego Mwile(216)
Nafasi ya Uwakilishi UVCCM ilichukuliwa na Upendo Lobay, alipita bila kupingwa, nafasi ya Wazazi imechukuliwa na Devotha Foste, (251)




