Msaidizi wa Askofu Daosisi ya Kaskazini Moshi Mkoani Kilimanjaro wa Kanisa la KKKT Mchungaji Dr Fredrick Shoo pamoja na wadau wengine wa elimu wakiangalia eneo la ujenzi wa shule katika kijiji cha Manga Kata ya Kasokola wilayani Mlele mkoani wa Katavi.
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Mpanda.
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kanisa la KKKT Usharika wa Kaskazini Mkoani Kilimanjaro na Arusha watembelea maeneo ya ujenzi wa shule ya sekondari katika kijiji cha Manga Kata ya Kasokolo wilaya ya Mlele Mkoani Katavi na kueleza nia ya kuvutiwa kuwekezakatika mkoa huo hasa eneo la Manga Kata ya Kasokola.
Wadau hao wa maendeleo walifika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mpanda kuonana na Kaimu Mkurugenzi Mwl.Naomi Nnko ambaye pia ndiye anayekaimu ukurugenzi katika wilaya ya Mpanda na Wilaya ya Mlele alieleza kuwa wawekezaji hao walifika ofisini kwake na kuomba kuja kuwekeza katika sekta ya elimu ambapo Mkurugenzi huyo alipokea wazo hilo la maendeleo na kulifanyia kazi kisha kuwapeleka wawekezaji kuonana na uongozi wa kijiji cha manga ili kupata Baraka na makubaliano ya kuridhia kutoa eneo litakalotumika kujengaa shule na kuwekeana mikataba.
Kwa upande wake Msaidizi wa Askofu Daosisi ya Kaskazini Moshi Mkoani Kilimanjaro wa Kanisa la KKKT Mchungaji Dr Fredrick Shoo akiwa na Katibu Daiosisi ya Arusha Ambele Mwaipopo walieleza nia yao kuja kuwekeza katika sekta ya elimu Mkoa wa Katavi.
Mbali ya wawekezaji hao pia wapo wadau wengine wa maendeleo ambao wanasaidiana na Halmsahauri ya Wilaya ya Mpanda kwa ajili ya kuwawesha kiuchumi na kielimu kwa kuwawekea miundo mbinu ya maji kwenye shule za msingi na sekondari zilizoko ndani ya makazi ya wakimbizi na shule kadha zile zilizoko nje ya makazi ya wakimbizi.
Mwakilishi wa shirika la kuhudumia wakimbizi Ofisi ndogo ya Mpanda Rose Mchina alieleza hayo alipotembelea na ujumbe wake ofisini kwa mkurugenzi mtendaji kueleza nia waliyonayo kwa ajili ya kuweka ushirikiano wa maendeleo katika sekta ya maji na elimu pia.
Aidha alieleza kuwa ushirikiano mwingine watajikita kusaidia katika kuwawezesha kiuchumi wananchi hususani vijana kutoka katika shule hizo kwa kuwajengea uwezo wa kujitegemea kwa kuwawesha kuanzisha miradi ya maendeleo ili waweze kuondokana na umasikini.
Mchina ameleza kuwa kwa kuanzia wataanza na shule mbili kutoka zilizoko makazini shule mbili za msingi ndani ya makazi ya Mishamo Wilayani Mpanda na mbili za sekondari ,pia shule mbili za sekondari zilizoko nje ya makazi ambazo ni mbili za msingi na mbili za sekondari.
Kwa upande wa wilaya ya Mlele Shule mbili za Msingi na sekondari mbili zilizoko ndani ya makazi ya Katumba na shule mbili za sekondari na mbili za msingi zilizoko ndani ya makazi na shule mbili za sekondari na mbili za msingi zilizoko nje ya makazi.
Shughuli ya awali kwa ajili ya uzitambua shule hizo imekwisha anza na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya alikwishaunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kushirikiana na wadau hao wa maendeleo kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambapo timu hiyo inaongozwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Mpanda Justini Tibendelana .




