MPIGANAJI MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AZIKWA TUKUYU

Rais wa UTPC Keneth Simbaya (kushoto) na waombolezaji wengine  wakiongoza waombolezaji walio fika Tukuyu, kubeba jeneza la marehemu  jana wakati ya mazishi ya Shujaa Daudi Mwangozi aliyekuwa Mwakilishi wa Kituo cha televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa aliyeuwawa kikatili wakati akishambuliwa na Polisi katika Vurugu za Chadema na Jeshi hilo akiwa anatekeleza majukumu yake ya kila siku ya utafutaji Habari. Shujaa Daudi Mwangosi alizikwa kijijini kwao Tukuyu Septemba 4, 2012.

Watoto wa marehemu wakiweka mashada ya maua juu ya kaburi la baba yako Kiopenzi Shujaa Daudi Mwangosi

Waombolezaji wakielekea makaburini kwa ajili ya kumzika marehemu Daudi Mwangosi jana huko Tukuyu.

 Rais wa UTPC Keneth Simbaya akiweka Shada la maua katika kaburi la Shujaa Daudi Mwangosi. Hii ndio safari ya mwisho ya mpendwa wetu Daud Mwangosi, Shujaa wa taaluma ya Habari aliyeuwawa wakati akitekeleza majukumu yake ya Uandishi wa habari mkoani Iringa.

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa uchungu wakati akitoa heshima za mwisho kwa mpedwa mumewe.

Umati wawatu uliofurika kumzika Shujaa Daudi Mwangosi.

Mjane wa Marehemu, Shujaa Daudi Mwangosi akilia kwa uchungu mkubwa huku akiwa amelala juu ya Kabuuri la Mpedwa Mumewake. Machozi ya  mjane huyu na watoto, Ndugu jamaa na marafiki wote wa Marehemu pamoja na Damu isiyo na hatia ya Daud Mwangosi katu havitaweza kupotea bure na Mungu atajibu kwa wale wote walio msababishia mama huyu na watoto wake wan ne kubaki wakiwa.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!