Watakiwa kuweka mbele matumizi ya vyanzo vya umeme

Mahmoud Ahmad Arusha

Nchi za SADC zimetakiwa kuweka ushirikiano na nguvu zake mbele kwenye sekta ya umeme ilikuweza kufanikiwa katika mikakati yake ya kuwasambazia wananchi umeme wa uhakika sanjari na kuvitumia vyanzo vya umeme kwa uhakika bila ya ubaguzi ili kuliondoa bara la Afrika kwenye kuomba teknojia hiyo kutoka kwa mataifa yalioendelea
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nishati na madini kwa hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo kwenye mkutano wa 39 wa mashirika 16 kutoka nchi kumi na mbili za kiafrika unaoendelea jijini Arusha.
 
Muhongo alisema kuwa tukiweza kuweka nguvu zetu kwenye ushirikiano wa vyanzo vya umeme na kuweza kuvitumia ipasavyo basi tutaondokana na dhana ya utegemezi wakati huduma hiyo kila siku inahitajika kwa maisha ya wananchi na ukuaji wa uchumi kwa mataifa yetu akawataka mashirika yote kutoka katika nchi hizo kukja na majibu sahihi ya kuondokana na tatizo la umeme wa mgawo kwenye nchi zetu.
 
“Umeme ni bidhaa ya uhakika na kila kila shirika linatakiwa kujiendesha kwa faida badala ya kupata hasara na kuleta visingizio visivyo na tija  kwani ni kudumaza maendeleo ya nchi zetu”alisema ,Muhongo
 
Nae mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo alisema kuwa mkoa wa Arusha unahitaji la megawatts 55 wakati tuna megawats36 na kutanabaisha kuwa umeme wa symbion ukimalizika utaweza kutatua tatizo la umeme kwa mkoa wa Arusha na kuwataka wafanyabiashara wa viwanda kuanza kusogea mkoani hapa kuwekeza kwani sasa Arusha ni mahali salama kwa uwekezaji.
 
 MulongoAlisema kuwa kwenye mataifa yetu kuna vyanzo vingi vya umeme ila  ushiriano unahitajika kati ya taifa na taifa hivyo tukishirikiana kuviendeleza tutatua tatizo la umeme kweye nchi zetu na baadae kwenye mataifa ya kiafrika na kuzinufaisha jumuiya zetu.
 
Akizungumza eng Declan Mhaiki alisema kuwa mkutano huo ni wa 39 na unashirikisha matifa 12 kutoka nchi zaq SADC na si mara ya kwanza kufanyika hapa nchini kwani wamekuwa na kubadilishana mkutano huo kutoka taifa moja kwenda jingine
 
Eng Mhaiki alisema kuwa pamoja na mengine watabadilshana uzoefu na kuweza kujadili kwa pamoja changamoto zinayoyakabili mataifa mbali mbali ya SADC juu ya suala zima la kuwekeza kwenye sekta ya umeme mfano mzuri ni umeme wa upepo wa Singida na sehemu nyinginezo zenye vyanzo vya umeme hapa nchini ilikuweza kuviendeleza
MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!