PSPF YATOA MCHANGO WA FLANA NA TRUCK SUITS KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MWENGE MKOANI RUKWA

Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Wakili Ileth Mawala akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya jumla ya flana 130 na Truck Suits 18 zitakazotumika kwenye shughuli ya kukimbiza mwenge Mkoani Rukwa ambayo itaanza tarehe 15-18, Septemba 2012. Mkuu huyo wa Mkoa alishukuru kwa zawadi hizo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo wa PSPF kwa kuchangia kwenye shughuli za maendeleo Mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.

Ujumbe ambao upo kwenye flana na truck suits hizo kama unavyosomeka hapo juu. Mbio za mwenge mwaka huu zinabeba ujumbe wa sensa ya watu na makazi pamoja na mabadiliko ya katiba. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!