TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)YAWAFANYIA SEMINA WANAHABARI

 Mkurugenzi Mkuu wa  Tume Ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Cosmas Msigwa (pichani) akisoma chapisho lenye maelezo  ya Kanuni mbalimbali za ajira na mahusiano kazini, ((Sept.7,2012) jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari ( hawapo pichani,) wakati wa semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu taratibu za kutatua migigoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi Tanzania.. ambapo wanahabari kupitia vyombo vyao waweze kusaidia kutoa elimu hii kwa  waajiri na waajiriwa pamoja na jamii nzima ya watanzania kwa ujumla kupitia vyombo vyao.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mdau wa Habari kutoka (UPL) Noor Shija (mwenye kitenge ) akichangia katika semina ya siku 1 kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (Sept 7,2012) kuhusu Taratibu za kutatua migogoro   ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi Tanzania.( Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Baadhi ya wanahabari wakipitia makabrasha katika semina ya siku moja jijini Dar es Salam kuhusu taratibu za kutatua mogogoro ya kila siku na changamoto zake  sehemu za kazi. Semina hiyo imeandaliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)  Wizara ya Kazi na Ajira , ambapo CMA imeeleza  tangu kuzinduliwa kwa TUME mwaka 2007 hadi -30 juni,2012 tume imepokea migogoro 43,003 na kati ya hiyo migogoro 31,125 sawa na asilimia 72.3 imeshapatiwa ufumbuzi.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)
Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya Usuluhishi na Maamuzi (CMA) (katikati mwenye suti) akiongea na waandishi wa habari jiji leo Dar es Salaam katika semina ya siku moja kwa wanahabari kuhusu taratibu za kutatua migogoro ya kila siku na changamoto zake sehemu za kazi Tanzania, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni  taasisi ya Serikali iliyoundwa chini ya sheria ya Taasisi za kazi na .7 ya mwaka 2004. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!