Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dr Hussein Mwinyi, anatarajia kuzindua mashine ya kisasa ijulikanayo kama MRI yaani ( magnetic resonance Imaging) inayotumika kupiga picha za sehemu za ndani ya mwili wa binadamu kama CT SCAN, X- RAY na vipimo vingine vya ndani ya mwili ya binadamu.
Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za hospitali hiyo ya TMJ, mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dr Parul Chhaya, amesema TMJ imefikia uamuzi huo wa kununua kifaa hicho adimu hapa nchini ili kuanza kutoa hudua hiyo adimu ambyo imekuwa tatizo kubwa hapa nchini, hali ambayo imekuwa ikiwalazimu watanzania wengi kusafiri kwenda nje ya nchi kwa matibabu yanayohitaji kifaa hicho na wakati mwingine watanzania wengi wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya kifaa hicho kwa mda unatakiwa.
“TMJ tumeona kuwa kuna sababu ya kuongeza vifaa muhimu katika huduma zetu za kila siku na kwasababu kadri siku zinapozidi kwenda tunakutana na changamoto mbalimbali hasa la wagonjwa wanahitaji huduma ya haraka ili kuokoa maisha yake, basi tukaona kwamba kuna sababu ya kujipanga kila siku ya mungu tukiweka malengo muhimu ya kuongeza vifaa muhimu kama hii mashine ambayo waziri wetu wa afya na ustawi wa jamii Dr Hussien Mwinyi anatarajia kuja kutuzindulia tayari kabisa kuanza kazi ya kuwasaidia watanzania wanaopata matatizo yanahitaji huduma ya kifaa hichi” alisema Chhaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa hospitali hiyo Bw. Arrwa Jaffji amesema kuwa TMJ imekuwa mtari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wagonjwa na wateja wake hali ambayo imefanya hospitali hiyo kuaminiwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF na kuitunuku cheti rasmi cha kuwahudumia wagonjwa wa bima ya afya mnamo mwaka 2011, na mpaka sasa hospitali hiyo inahudumia wagonjwa zaidi ya 2000 wa magonjwa mbalimbali kwa siku moja.
“Tunatambua umuhimu wa afya ya mwili ambayo ndio huduma inayotolewa na TMJ na kwasababu hiyo tumekuwa tukipambana kwa kila hali kuhakikisha kwamba tumapambana mpaka leo tumefanikiwa kupata hiki kifaa ambacho watanzania wengi wanapoteza maisha kutokana na kukosa huduma ya kifaa hiki na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia watnzania wote wanaotuzunguka kwamba sasa huduma ya CT SCAN itakuwa inatolewa hapa TMJ mara tu baada ya uzinduzi wa kifaa hicho adimu hapa nchini” alisema Dr Jaffji.
Hospitali ya TMJ itakuwa kituo cha pili cha afya kuwa na kifaa hicho ikiwa imetanguliwa na hospitali ya Aga Khan kwa upande wa hospital binfsi na ya tatu Tanzania nzima ikitanguliwa na hospitali ya taifa ya muhimbili.
TMJ imekuwa hospitali binafsi pekee inayoendesha huduma ya chanjo ya polio kwa watoto wenye umri kuanzia 0 miaka 9 bure kila mwaka.




