FFU wa Ngoma Africa band kutumbuiza AFRIKA-MESSE,Bremen,Ujerumani

Pia watapeleka Mzuka ndani ya Bremerhaven festival, 12.09.2012
 
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU,
yenye maskani yake kule ujerumani,bendi hiyo inayokamatia taji la kimataifa la
“IDA-International Diaspora Award’ inatarajiwa kutumbuiza katika maonyesho
mengine makubwa siku ya jumatano 12.09.2012 itakua mjini Bremerhaven, na
Jumamosi ya 15.9.2012 Kikosi kazi hiko kitapeleka nguvu zote katika maonyesho 
makubwa ya biashara ya kiafrika “AFRIKA-MESSE” Bremen,yatakayafanyika
mjini Bremen,Ujerumani.
Bendi hiyo inayotamba CD mpya “Bongo Tambarare” ambayo imeshatua kwa
kishindo katika vituo vya redio mbali mbali ndani na nje.
Ngoma Africa band iliyoanzishwa mwaka 1993 muhasisi wake Kamanda Ras Makunja,
 wa FFU,ambaye pia ndiye kiongozi wa kikosi kazi hiko.
Kikosi kazi hiko kilichojizolea washabiki kila kona duniani kimekua tishio
la kimataifa,inasemekana kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika iliyo fanikiwa
kuteka nyoyo za washabiki wa kimataifa na kuwafanya washabiki kuwa
ndio wamiliki wa bendi hiyo.
Usikose kuwasikiliza bofya hapa www.ngoma-africa.com 

Ungana nao hapa www.twitter.com/thengomaafrica

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!