WASAFIRI JIJINI DAR ES SALAAM WASOTA VITUONI KWA KUKOSA USAFIRI WA MABASI

BAADHI ya wasafiri wa jiji na wale wanaotumia barabara ya Morogoro kwenda mikoani juzi walitaabika kwa kukaa vituoni hadi usiku mwingi wakisubiri kusafiri kurudi majumbani kwao bila mafanikio kutokana daladala na gari nyingine kutooneka vituoni bila sababu.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Fullshangweblog jijini Dar es Salaam jana, wasafiri hao, walisema Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), ingilie kati na kuwachukulia hatua madereva wote wanaojiingiza na tabia yakukatisha njia na kuyaelekeza magaari wanakotaka.
 
Walisema miongoni mwa abiria waliotaabika kutokana na vitendo hivyo vya kutotii sheria vilivyofanywa na madereva wa daladala na wale wa gari za shamba, ni wale  wanaoishi maeneo ya Kimara Mbezi na Kibaha.
 
Mmoja wa wasafiri hao, Said Mahadulah alisema hali iliyojitokeza juzi hadi jana ilikuwa sawa na mgomo kutokana na gari husika kutoonekana vituoni kwa makusudi.
 
“Unajua juzi ilikuwa hatari baada ya daladala zote kama vile zilikubaliana kwa makusudi kuwakusanya wasafiri na kwenda  kuwatelekeza paele Ubungo hali iliyofanya mlundikano katika kituo kile kufikia zaidi ya watu 1000 ambapo ilikuwa hatari kubwa”alisema.
 
Mahadulah alisema miongoni mwa watu waliyoteseka walikuwa wakina mama ambao walikuwa wakisafiri huku wakiwa na watoto usiku ule wa balaa.
 
Alisema vitendo hivyo ni mwuendelezo wa madereva hao ila juzi walijaribu jaribio jipya ambalo kama likiachwa liendelee latweza kuleta mgogoro usioeleweka hatima yake nini.
 
Naye Joyce William, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea Kibaha akiambatana na watoto wake wanne alisema hata isahau siku hiyo jinsi alivyoteseka na wanawe ambao walikuwa wakilia hovyo wakitaka kulala bila mafanikio.
 
Alisema alifika Ubungo saa 1:30 usiku hata hivyo, alishindwa kupata usafiri hadi saa sita usiku alipoamua kutafuta nyumba za kulala wageni ambako alikwenda kulala na wanawe.
 
Joyce alisema kuna ulazima kwa Mamlaka husika kuyafanyia kazi maoni ya wananchi katika kuwadhibiti madereva wa daladala na wengine ambao tayari wamekwisha jijengea uhalali kuwa nyakati za usiku wanauwezo wakufanya chochote kwa madai kuwa serikali imekwenda kulala.
MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!