Shirikishi la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 17/09/2012.
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke,Kinondoni na Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali umejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).









