NHIF YAPONGEZWA KWA HUDUMA NZURI NA ZA HARAKA

Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma akimpa kipande cha keki mmoja wa wanachama aliyekuwepo wakati wa tukio hilo.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Beatus Chijumba akipokea keki kutoka kwa Imran Dhalla ambaye ni Mwanachama aliyeridhishwa na huduma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Beatus Chijumba akipokea keki kutoka kwa Imran Dhalla ambaye ni Mwanachama aliyeridhishwa.

Keki iliyotolewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mjumbe wa Central Board of Education (CBE) Imran Dhalla ambaye ameridhishwa

Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma akimpa kipande cha keki mmoja wa wanachama aliyekuwepo wakati wa tukio hilo.

Kutokana na huduma nzuri zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), mmoja wa wanachama wa Mfuko huo, Imran Dhalla ambaye pia ni Mjumbe wa Central Board of Education (CBE) amefika katika Ofisi za Mfuko huo na kuupongeza kwa huduma nzuri na za haraka alizozipata.

Imran ambaye alikabidhi keki kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Beatus Chijumba kama ishara ya kuridhishwa na huduma alizopata, alisema ushirikiano mkubwa alioupata ndio umemsukuma kuandaa keki hiyo na kufika ofisi za Mfuko huo kwa lengo la kuushukuru.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Beatus Chijumba akipokea keki hiyo, alitoa mwito kwa wanachama kuupatia mfuko huo mrejesho wa huduma wanazopata ili uweze kuboresha zaidi.

“Mfuko uko tayari kupokea mrejesho wa aina yoyote, uwe mzuri au unaotutaka kuboresha zaidi…tunawaomba na wanachama wengine kuiga mfano huu ambao tunaamini utatusaidia sana kuboresha huduma zetu,” alisema.

Imran alisema kuwa wafanyakazi wote wa mtandao wa shule za Al Muntazir wamejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na mchakato unaendelea wa kuhakikisha jumla ya wanafunzi 3,800 wanajiunga na Mfuko huo ili wawe na uhakika wa matibabu.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!