WAANDISHI WA HABARI WAANDAMANA JIJINI DAR ES SALAAM, NI KUHUSU KIFO CHA DAUDI MWANGOSI

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena akizungumza mara baada ya waandishi wa habari kumaliza maadamano yao ya Amani kutoa ujumbe wao kwa jeshi la Polisi kutokana na kupoteza maisha kwa  mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi aliyeuwawa katika vurugu kati ya Polisi na Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kijiji cha Nyololo Mkoani Iringa hivi karibuni, Maandamano hayo yalianzia katika ofisi za kituo cha Televisheni ya Chanel Ten ambako marehemu alikuwa mwakilishi wake mkoani Iringa na kuishia katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam leo asubuhi.

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

Waandishi wa habari mbalimbali wakitoa dukuduku zao mara baada ya kumalizika kwa maandamano hayo leo asubuhi.

Mwandishi wa habari Mkongwe Bw Jackton Manyerere akizungumza katika maadamano hayo kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam
Waandishi wa habari mbalimbali wakiwa wamejikusanya katika ofisi za Chanel Ten kabla ya kuanza kwa maandamano hayo leo asubuhi.

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Bw. Neville Meena akitoa ratiba ya njia ambazo maandamano yatapita kabla ya kuanza kwa maandamano hayo wanaofuatia katika picha ni Profesa Rwaitama, Jane Mihanji na Rashid Kejo.

Waandishi wa habari wakiandamana huku wakiwa wamebeba picha ya marehemu Daudi Mwangosi.

Maandamano yakiendelea kupitia mitaa kadhaa  jijini Dar es salaam

Hapa yakiwa yamefikia katika barabara ya Morogoro kuelekea Jangwani.

Polisi walikuwepo kuhakikisha usalama

Mdau Maximilian kutoka kituo cha Televisheni cha Mlimani TV.

Waandishi wa habari wakiigiza vurugu zilizotokea  mkoani Iringa ambapo Mwandishi wa habari Marehemu Daudi Mwangosi alipoteza maisha katika vurugu hizo.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!