BENKI ya CRDB kupitia tawi lake lililoanzishwa Juni mwaka huu, lililopo Tegeta jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kuvuna wateja wapya zaidi ya 400.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja wa tawi, Daudi Nyandwi, alisema wateja hao ni wa makundi mbalimbali.
Nyandwi alisema, kabla ya tawi kuwepo wateja na Wananchi wengine walikuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda Mlimani City na sehemu nyingine kwa ajili ya kupata huduma za kibenki.
Hivyo, kufunguliwa na kufanyakazi kwa tawi hilo kumesaidia wateja na Wananchi kwa ujumla kupata huduma za kibenki kama kawaida kama vile; kutoa, kuhamisha na kuweka fedha, mikopo na kupata huduma za kibenki kwa njia ya mtandao wa Intaneti.
Alitaja huduma zingine kuwa ni huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi na mashine mbili za kutoa fedha kwa saa 24.
Hata hivyo baadhi ya wateja ambao waliongea na www.fullshangweblo.com walisema CRDB bado ina changamoto kubwa ya kutoa elimu kuhusiana na huduma zake mpya ambazo wamezianzisha ili wateja wazielewe.
Walisema wateja wanahitaji elimu ya kina juu ya baadhi ya huduma ili wazitumie kuendana na mazingira.









