MTUHUMIWA WA KIFO CHA MWANGOSI AFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Marehemu Daudi Mwangosi enzi za uhai wake.

…………………………………………….

NA MWANDISHI WETU – MAELEZO 

 WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel  Nchimbi  amesema askari anayetuhumiwa  kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10,  marehemu Daudi Mwangosi amefikishwa mahakamani  leo.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo iliyosainiwa na Waziri Nchimbi ilieleza kwamba  Septemba  7,mwaka huu  alikabidhiwa taarifa ya  awali ya uchunguzi wa polisi  juu ya kifo cha mwandishi huyo   na  Mkuu wa Jeshi la  Polisi,  Inspekta  Jenerali Said Mwema.

Hivyo  Septemba  11, mwaka huu  aliliagiza Jeshi la Polisi kumpeleka  mtuhumiwa huyo askari  namba G. 2573 PC   Pasifious  mahakamani  leo kama ilivyotakiwa ma Mkurugenzi wa Mshtaka(DPP).

 Waziri Nchimbi alisema wakati mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani , kamati iliyoundwa chini ya Jaji Ihema itaendelea na kazi yake ili kupata suluhisho la kudumu la migongano ya kikazi kati ya polisi na waandishi wa habari na waandishi wa habari, polisi na vyama vya siasa ikiwemo kuboresha mahusiano  zaidi kati ya polisi na raia.

 Aliongeza kuwa mkondo wa sheria umeanza kufuatwa  nawaomba wadau wote kutoa nafasi  kwa  utaratibu huo wa kisheria kufanya kazi.

Aidha aliongeza kuwa  uchunguzi huo wa awali ulibaini mambo makubwa mawili ,ambayo ni mlipuko uliotokea ulitokana na bomu la Machozi na bomu hilo lilifyatuliwa na askari huyo.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!