Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) kwa kupitia chama cha waamuzi wa ngumi za ridhaa wameteua na kuwathibitisha waamuzi watakao tumika katika mashindano ya ubingwa wa taifa yatakayofanyika kuanzia tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa taifa wa ndani.
Waamuzi walioteuliwa ni:-
Mohamed Kasilamatwi mwamuzi wa kimataifa na Juma Selemani mwamuzi wa Afrika kama wasimamizi wa waamuzi.
Waamuzi wa ngazi ya taifa walioteuliwa ni:-Maneno Omari, Ridhaa Kimweli, Mohamed Bamtulla, Shija Masanja, , Moshi makali, Hamza abdallah na Marko Mwankenja.









