MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA PINDA MAGU

Shamba la kilimo cha umwagiliaji cha Mbogamboga la Ngongoseke lililoko katika kijiji cha Nsola wilayani Magu ni mfano wa kuigwa katika  matumizi ya ziwa Victoria. Pichani, nyanya ndogondogo maarufu kwa jina la nyanyapori zikiwa zimelimwa kitalaam kwenye shamba hilo ambalo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilitembelea Septemba 13, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mtoto akiwa  amenyanyuliwa juu ili aweze kumwona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa Sabasaba Mjini Magu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Septemba 13, 2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua gati la kupokelea samaki katika kijiji cha Kigangama wilayani Magu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Septemba 13, 2012.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!