Aqua Well Drilling ya jijini Dar es salaam yaendelea na kazi ya uchimbaji wa visima vya maji vijijini

Mafundi wa kampuni ya kuchimba visima virefu ya Aqua Well Drilling ya jijini Dar es salaam Jerry Timoth kushoto na Nassor Ahmed wakisafisha maji kwenye kisima, mara baada ya kukamilisha uchimbaji na kufunga pampu ya kupandisha maji, hatua hiyo pia hutumika kutambua kiwango cha maji kilichopo katika kisima hicho na kusafisha maji , katika picha watoto wakifurahia na kuchota maji katika kisima hicho katika mji mdogo wa Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro , Mradi huo umegharimiwa na World Bank kwa pamoja na michango ya wananchi katika mji huo.

Akina mama wakichota maji katika kisima kifupi kilichokuwa kikitumiwa na wakazi hao kabla ya kuchimba kisima kipya ambacho ni kirefu zaidi na kinatoa maji baridi.

Mtoto ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa na baiskeli huku akiwa amebeba madumu ya maji akielekea kuchota maji katika kisima hicho katika mji wa Dumila.

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!