Tumefika salama mjini Morogoro mjini kasoro bahari tukitokea mkoani Dodoma amabako jana kulikuwa na tamasha kubwa kabisa la Serengeti Fiesta 2012 lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, hapa tuko Dumila kutoka kushoto ni Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager Dereva wetu Ammanuel Mligi na Askari wa miamvuli Johna Bukuku Mkurugenzi wa Fullshangweblog tukiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Moro.
Jumapili nitaelekea Iringa ambako jumatatu kutazinduliwa wiki ya Nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Iringa.
Kutoka kushoto ni Dereva wetu Emmanuel Mligi, Askari wa miamvuli Ahmed Michuzi au Michuzijunior kama anavyojulikana mkurugenzi wa Jiachieblog na Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager.




