SIMBA YAINYUKA AFRICA LYON MAGOLI 3-0 KWENYE UWANJA WA TAIFA

Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam imefanikiwa kuanza vyema ligi kuu ya Vodacom baada ya kuibanjua timu ya Afican Lyon magoli 3-0 kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo, magoli ya timu ya Simba yamefungwa na wachezaji wake mganda Emmanuel Okwi, Mrisho Ngasa na Nassor Chollo.

Kwa matokeo ya leo ina maana kwamba timu ya Simba inaaza ligi hiyo ikiwa na pointi tatu na magoli matatu ukiwa ni mtaji tosha kwa kuanza, wakati huohuo mahasimu wao wakubwa timu ya Yanga ya Jangwani kutoka jijini Dar es salaam ilikuwa na kibarua kigumu kule mkoani Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine , wakati ilipokutana na timu iliyopanda daraja ya maafande wa Magereza “Prison”, katika mchezo huo matokeo yamekuwa 0-0 baada ya maafande hao kukaza buti na kuwazuia wana Yanga kwenye uwanja wa nyumbani kwao

MIMI NI MPIGA PICHA NA MWANDISHI WA HABARI WA KUJITEGEMEA NA KUPITIA BLOG HII NINA IMANI TUTAWEZA KUPEANA HABARI MBALIMBALI ZA BURUDANI ZITAKAZOFURAHISHA NA KUELIMISHA NAOMBA USHIRIKIANO WENU ILI TUWEZE KUFIKA TULIPOKUSUDIA

Got something to say? Go for it!