Kaimu mkurugenzi wa Chakula bora (food safety) Bw, Martin Rimanya akimueleza waziriwa Afya na Ustawi wa jamii Dk Hussein Mwinyi aina ya vyakula walivyo vifanyia uchunguzi ambapo amesema kuwa kuna jumla ya vyakula 3018 ambavyo vimesajiliwa baada ya kufanyiwa uchunguzi na pia amesema kuwa kuna majengo 5025 ambayo yapo tayari kukagua vyakula nchini na kuongeza kuwa watu na makampuni , yanayotakiwa kuingiza chakula nchini ni watu 1431 tu. Aidha Bw, Rimanya ameongeza kuwa wamefanya uchunguzi katika mikoa kumi ili waweze kubaini ni watu kiasi gani walio athirika na sumu inayopatikana katika vyakula zinazotokana na ukungu maarufu kama sumu kuvu na kubaini kuwa Mkoa wa Iringa umeathiriwa zaidi na sumu hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Dawa na Vipodozi TFDA Bw, Henry Irunde akimwonyesha Waziri wa afya Dr. Hussein Mwinyi document inayoelezea majaribio ya dawa mbalimbali zikiwemo dawa za kienyeji.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamhii Dr. Hussein Mwinyi akimsikilza maelezo kutoka kwa maofisa wa TDFA.








