Halmashauri yawilaya ya Meru imefanikiwa kupima viwanja 40000 na kuviweka katika michoro na ramani ili wananchi waweze kuishi katika makazi bora nay a kisasa.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Goodson Majola wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani.
Majola amesema kuwa bado zoezi hilo linaendelea ambapo kwa sasa wataelekea katika mji wa usa ili kuweza kuwapimia ardhi na waweze kupatiwa hati miliki na kumiliki ardhi kisheria.
Aidha ameongeza kuwa lengo la kupima ardhi ni ili wananchi waweze kuishi katika makazi ya kisasa na yaliyopangwa kwa kuwa maendeleo ni haki yao na kupunguza ujenzi holela.
Pia Majola amesema kuwa ni lazima wananchi waoneshe ushirikiano wa karibu ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuwa nia na malengo ni kuwamilikisha ardhi yao kisheria.
Vilevile amesema kuwa ni lazima Mkurugenzi na timu yake ijipange ili iweze kutoa taarifa kwa wananchi husika tena ziwe sahihi ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.
Majola amesema kuwa kazi hiyo inaendeshwa rasmi na kampuni ya Ardhi Plan na ni lazima wananchi wote wa wilaya hiyo wapimiwe ardhi ili wamiliki kisheria kwa kuwa kuondoa migogoro ya ardhi.
Hata hivyo amewataka wananchi kutambua kuwa pindi wanapopimiwa ardhi kuna faida kubwa ikiwemo ya kukopa katika taasisi mbalimbali za mikopo kwa kuwa ardhi zao zitakuwa zinatambulika kisheria.









